Mpango wa Mungu katika maisha yakoMfano
Kunatokea nini tunapokuwa hatuoni mpango wa Mungu?
Katika Agano la Kale, Yeremia alikuwa nabii akiwakilisha ujumbe wa Mungu kwa watu wake ambao walikuwa utumwani Babeli. Hapo siyo mahali walipotakiwa kuwa. Haukuwa ndiyo mpango. Badala ya Mugu kuwakomboa moja kwa moja, anawaambia "kujenga nyumba na kukaa ndani yake". (Yeremia 29:5) na “kuutakia amani …mji ule ambao nimewafanya mkachukuliwe mateka.” (Yeremia 29:7 )
Mistari michache baadaye, Mungu anasema,… “Mtakuwepo Babeli kwa miaka sabini. Ndipo nitawajilia ninyi, na kulitimiza neno langu jema kwenu, kwa kuwarudisha mahali hapa". Yeria 29:10
Miaka sabini! Wengi wetu siyo wavumilivu kusubiri kitu kwa sekund 70, acha miaka 70.
Yote hayo ni kwa muktadha wa mstari unaofuata ambao yawezekana umeusikia: “Maana nayajua mawazo ninayowawazia," asema Bwana. Ni mawazo ya amani wala si ya mabaya, kuwapa ninyi tumaini siku zenu za mwisho". Jeremiah 29:11 NLT
Kuna mambo matatu kuhusu mpango unayotakiwa kuyajua.
1.) Mipango mizuri inaweza kuchukua muda. Mungu aliwaambia wana wa Israeli watakuwa utumwani kwa miaka 70. Wat wengi waliokuwa wanasikiliza hawataweza kuona upande wa pili wa ahadi hiyo. Wakati mwingine inaweza kuonekana inachelewa kwa Mungu kuufunua mpango wake kwako. Ukweli ni kwamba unaweza usione matokeo kamili ya kile Mungu alichonacho kwa maisha yako-kinaweza kutokea kwa vizazi mbele yako na usijue!
2.) Nyakati za kusubiri si nyakati zilizopotea. Angali kwamba Mungu hakuwaambia wana wa Israeli kusubiri tuu kwa miaka sabini bila kufanya kitu. Aliwaambia wautakie amani na mafanikio mji ule aliowatuma. Popote ulipo sasa hivi, Mungu anaweza kukutumia! Usiache kuleta mabadiliko changa kwa ajili ya ufalme sasa kwa kusubiri majira ambayo Mungu hajakuweka.
3.) Mipango yake ni mizuri. Katika majira yoyote unayojikuta upo sasa, ahadi ya Yeremia 29:1ni kweli: Mungu anamipango mizuri kwako—mipango ya tumaini siku za mwisho. Yawezekana mambo hayaenda sawasawa sasa hivi, utaona mema upande mwingine.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Je, nini mpango wa Mungu juu ya maisha yako? Ni maswali ya kawaida tuliyonayo wote kama wafuasi wa Kristo. Ila kama tukiwa waaminifu, wazo la mpango wa Mungu katika maisha yetu linaweza kuwa gumu kwetu. Katika siku hizi 6 za mpango wa kujisomea Biblia, tutajifunza jinsi mpango wa Mungu usivyo mgumu kama tunavyoweza kufikiri, ila ni mwema kuliko tunavyoweza kufikiria
More