Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Mpango wa Mungu katika maisha yakoMfano

God’s Plan For Your Life

SIKU 1 YA 6

Mpango wa Mungu unaweza usiwe mgumu kama unavyodhani.

Ulishawahi kusikia kwamba Mungu "anampango katika maisha yako"? Mara nyingi, wazazi wetu na wakubwa wanaotuwazia mema huongea kuhusu mpango wa Mungu wakitutia moyo, ila kama tu waaminifu, wakati mwingine inaishia kututisha! Lakini jambo ni hili: mpango wa Mungu hauko mgumu kama unavyodhani.

Katika Agano la kale, kuna hadithi ya mtu aitwaye Abram. Mwanzo 12:1 inasema Mungu alimwambia Abram aondoke kutoka kwenye nchi yake aliyozaliwa na aende mahali ambapo atamwonyesha.Kuondoka kwenye nhi uliyozaliwa, nyumbani kwenu, kwenda sehemu usiyoijua bado? Hiyo inatisha sana! Bado katika Mwanzo 12:4, inasema kwamba "...Kwa hiyo, Abramu akaondoka kama Mwenyezi-Mungu alivyomwamuru; ...."

kila kinachofuata ambacho alitaka afanye.

Na kukudokeza tu: Kwasababu ya utiifu wake, Mungu baadae alibadili jina lake kutoka Abram kuwa Abraham, likimaanisha "baba wa wengi". Na Abraham akaenda kuwa baba wa mataifa mengi! Abraham anaonekana tena kwenye Waebrania 11 katika orodha ya majina ya wenye imani katika Biblia. Ni vyema sana hii, sio?

Abraham ni mfano mzuri kwa mtu anayeishi kwa imani- hata pale anapoona tu sehemu ndogo ya mpango wa Mungu katika maisha yake. Ni hakika hakuwa kamili, ila maisha yake yalijawa na wakati ambapo alimwamini Mungu, hata pale tunapoona haieleweki.

Sasa, inapokuja kwenye mpango wa Mungu kwenye maisha yetu, mara nyingi ndivyo Mungu anavyofanya kazi-anaongea nasi kupitia Neno Lake (Biblia) na kutupa muongozo katika hatua zifuatazo. Hivyo ndivyo mpango wa Mungu ulivyo. Ni mfuatano wa hatua zifuatazo tunazochukua tukiwa na utiifu kwa Mungu.

Zaburi 119:105 inasema kwamba Neno la Mungu ni taa ya miguu yetuna ni mwanga wa njia zetu.Mstari wa kwanza hauongelei aina ya taa uliyonayo chumbani kwako ambayo inaleta mwanga katika chumba chote. Ila, mstari huu unaongelea ule mshumaa mdogo. Hautatoa mwanga mkubwa-kidogo tu kuonyesha kilicho mbele yako. Itakua kama kwenda kwenye chumba chenye giza tororo na tochi ndogo kabisa-unaona tu hatua chache mbele.

Kama Abram, Mungu hatatupa mpangilio mzima wa maisha yetu. Kama angetupa, usingekua na sababu ya kuishi kwa imani na uaminifu kwake! Badala yake, Mungu anataka aseme nasi kupitia Neno Lake na Wakrito waaminifu katika maisha yetu ili atusaidie kwenye mpango ufuatao--hatua moja baada ya nyingine.

siku 2

Kuhusu Mpango huu

God’s Plan For Your Life

Je, nini mpango wa Mungu juu ya maisha yako? Ni maswali ya kawaida tuliyonayo wote kama wafuasi wa Kristo. Ila kama tukiwa waaminifu, wazo la mpango wa Mungu katika maisha yetu linaweza kuwa gumu kwetu. Katika siku hizi 6 za mpango wa kujisomea Biblia, tutajifunza jinsi mpango wa Mungu usivyo mgumu kama tunavyoweza kufikiri, ila ni mwema kuliko tunavyoweza kufikiria

More

Tungependa kushukuru huduma ya LifeChurch.tv kwa kutoa mpango huu. Kwa maelezo zaidi, tafadhali tembelea: www.life.church