Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Mpango wa Mungu katika maisha yakoMfano

God’s Plan For Your Life

SIKU 3 YA 6

Unagunduaje mpango wa Mungu kwa ajili ya maisha yako? 

Kama umewahi kushiriki mashindano ya mbio, unajua ni muhimu kutunza mwendo sahihi. Kama ukienda taratibu, utabaki nyuma kirahisi na watu watakupita. Ukienda mbio zaidi, unaweza kuchoka haraka na usiwe na nguvu hata ya kumaliza mashindano. 

Kupata mwendo sahihi ukiwa unakimbia inaweza kuwa changamoto. Bahati nzui, inapokuja kwenye maisha yetu ya kikristo, tuna mtu anayewekea mwendokwa ajili yetu. 

Wagalatia 5:25 inasema “ishi kwa Roho na enenda kwa Roho” 

Kama tulitakiwa kuenenda kwa Roho, ina maana Roho Mtakatifu anatuwekea mwendo. Tusibaki nyuma au kwenda mbele zaidi- tunatakiwa kwenda kwa hatua.

Tunapobaki kuenenda kwa Roho, anatupa hekima na ufahamu ili utusaidie katika maamuzi yetu. Mithal 3:6 inasema kwamba tunapomkiri yeye, naye anayoosha mapito yetu.

Sawa, yote inaonekana ni nadharia nzuri. Lakini tuna enendaje katika Roho?

Hapa kuna njia tatu za kuanza:

1.) Mtafute Bwana kupitia neno lake.Kwa sababu unasoma mpango huu wa Biblia katika App ya Biblia, hakika uko kwenye ya kufanya hivyo tayari! fanya kuwa desturi kusoma neno la Mungu kila siku. Kuna mipango mingi ya Biblia unayoweza kuanza nayo, na kama unataka kuwajibika, unaweza kufanya katika vikundi vidogo vidogo, pia!

2.) Omba mara kwa mara. Usiache suala la maombi likutishe. Maombi ni kusema na Mungu tuu, na kisha kumsikiliza. Kama unasumbuliwa kirahisi (kama wengi tulivyo), inasaidia kufungua sehemu ya kuandikia kwenye simu yako na kuandika yote unayotaka kuombea.

3.) Kaa katika jamii.Kuenenda katika Roho maana yake kuzungukwa na watu wenye mawazo kama yako ambao wanamfuata Kristo. Njia bora ya kufanya hivyo ni kudumu katika kundi lako dogo na kuhudhuria kanisani mara kwa mara. Hata kuzidi: anza kutumika kanisani. Utakutana na watu wapya na kujenga urafiki na wakristo wengine.

siku 2siku 4

Kuhusu Mpango huu

God’s Plan For Your Life

Je, nini mpango wa Mungu juu ya maisha yako? Ni maswali ya kawaida tuliyonayo wote kama wafuasi wa Kristo. Ila kama tukiwa waaminifu, wazo la mpango wa Mungu katika maisha yetu linaweza kuwa gumu kwetu. Katika siku hizi 6 za mpango wa kujisomea Biblia, tutajifunza jinsi mpango wa Mungu usivyo mgumu kama tunavyoweza kufikiri, ila ni mwema kuliko tunavyoweza kufikiria

More

Tungependa kushukuru huduma ya LifeChurch.tv kwa kutoa mpango huu. Kwa maelezo zaidi, tafadhali tembelea: www.life.church