Mpango wa Mungu katika maisha yakoMfano
Sheria tatu zisizoandikwa za mpango
Hebu angalia hili: Unanunua shati jipya ambalo una hamu ya kulivaa shuleni kwa sababu unajua ni kitu ambacho mwishowe kuna mtu atakutambua. Unapanga nguo utazovaa ambazo unajua zitashabihiana sawasawa. Unapokula chakula cha mchana, jambo linatokea: unajimwagia mchuzi shati jipya lote—kama ambavyo umetarajia kukutana na mtu siku zoteghafla anakuja mezani kwako.
Wakati mwingine, maisha hayaendi kama ulivyopanga.
Katika Biblia, kuna habari ya mtu anayeitwa Gidioni. Si tuu kwamba Gidioni alitoka kwenye kabila dogo kwenye uzao wa Manase bali pia alikuwa mtu mdogo katika familia yake. Hakutarajiwa hata kuchaguliwa na Mungu. Baadaye, Mungu anamuongoza Gidioni vitani na wamidiani, kabila la maadui, lenye askari 38,000. Ndipo, Mungu anamwambia Gidioni ana askari wengi, na kama wakiwapiga wamidiani, itaonekana wamewapiga wao wenyewe. Kwa hiyo, Gidioni akawatuma askari 20,000 nyumbani. Mungu akamwambia bado ni wengi, mwishowe, Gidioni akabakiwa na askari 300. Bwana anampa Gidioni ushindi dhidi ya wamidiani akiwa na askari 300- kitu ambacho kwa uhakika sicho Gidioni alichokipanga mwanzo.
Tunapofikiria mbeleni na kile Mungu alicho nacho kwa ajili yetu, ni muhimu kukumbuka kwamba vitu siku zote haviwezi kwenda kama tunavyopanga.
Ki ukweli, kuna sheria tatu zisizoandikwa unatakiwa kuzifuata:
1.) Panga kuanza upya. Maisha ni mtiririko wa kuanza upya. Mara unapomaliza shule ya kati, ni wakati wa kuanza shule ya juu. Mara unapokuwa umemamliza shule ya juu, ni wakati wa kuanza kujiandaa na chuo na kuwa mtu mzima. Ukweli ni kwamba, humalizi. Jifunze kuanza upya. Wakati mipango inapobadirika, nenda nayo. Huwezi kujua Mungu amekupangia nini. Pokea wakati ulionao sasa hivi.
2.) Panga kusema hapana. Wakati mwingine, tunakiwa kusema "hapana" kwa mambo mazuri ili kusema "ndiyo" kwa mambo bora zaidi. Hatuwezi kufanya kila kitu. Omba hekima kujua wapi uwekeze muda wako mwingi ili kuwa na matokeo makubwa kwenye ufalme wa Mungu.
3.) Panga kuwa mbunifu. Mipango ya Munu wakati mwingine inaweza kutuchukua katika njia ambayo hatuitarajii. Kwa Gidioni, ilihusisha alivyokuwa navyo- vyombo vya udongo na miali ya moto badala ya silaha zilizo tayari kwa vita. Tumia karama alizokupa Mungu leo. Usijali watu wengine wana nini. Tambua kile ambacho Mungu amekupa kwa msaada wake kitaenda mbali zaidi kuliko unavyotarajia.
Kuhusu Mpango huu
Je, nini mpango wa Mungu juu ya maisha yako? Ni maswali ya kawaida tuliyonayo wote kama wafuasi wa Kristo. Ila kama tukiwa waaminifu, wazo la mpango wa Mungu katika maisha yetu linaweza kuwa gumu kwetu. Katika siku hizi 6 za mpango wa kujisomea Biblia, tutajifunza jinsi mpango wa Mungu usivyo mgumu kama tunavyoweza kufikiri, ila ni mwema kuliko tunavyoweza kufikiria
More