Ahadi za kila siku ya maisha yakoMfano
Mungu ataongoza safari yako
Maisha ya Kikristo yanaweza kulinganishwa na safari. Roho Mtakatifu ndiye kiongozi wetu ... Anatuongoza kila siku. Na Yeye daima anatuongoza katika kile kinachofaa kwa maisha yetu. Funguo la safari ya mafanikio na ya kufurahisha ni kumfuata.
Lakini kumfuata Mungu kunamaanisha nini? Kimsingi, inamaanisha kumtii, kufuata uongozi wake, na kufanya kile anachosema
Mara nyingi tunakimbia mbele ya Mungu. Tunaweza kufikiria tunajua mwelekeo bora wa kuchukua au tunakosa uvumilivu kwa muda wake na kuchukua hatua mbaya kwa vile inakaa ya haraka. Tatizo ni, tukigundua kuwa barabara hiyo inaongoza kwenye mwisho wa wafu, tutapaswa kurudi tena mahali ambapo tuliondoka kwenye njia mwafaka.
Habari njema ni, Mungu yuko pale, akisubiri kutuongoza tena na kutuonyesha njia sahihi ya kwenda.
Bwana amepanga vizuri safari ya kila mmoja. Tunahitaji kuelewa kikamilifu kwamba anatupenda, kwamba ni mwema na mwenye haki na tunaweza kumwamini
Tunaweza kumtegemea Yeye kutuongoza katika mwelekeo unaofaa kwetu. Tunaweza kumtegemea Yeye kutusahihisha tunapopotea na kutuongoza kwenye mahali pa haki. Tunaweza kumwamini yeye na wengine juu ya njia yetu. Tunaweza kumwamini Yeye kwa maisha yetu ... tosha!
Fuata mwongozo wa Roho Mtakatifu, kwa sababu Yeye anajua njia na atakuwa daima na wewe. Mwamini Yeye kukuongoza katika mema yote aliyopanga kwa ajili yako muda mrefu kabla hujazaliwa. Na ufurahie safari.
OMBI LA KUANZA SIKU
Mungu, Neno lako linasema kwamba Wewe huelekeza hatua za waumini. Ninaamini wewe unaniongoza kwenye safari uliyonayo kwa ajili yangu, na najua kwamba nitakapotoka kwenye njia, utakuwa daima nami kunisaidia kurudi na kuendelea.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Mungu ametupa ahadi tele ambazo tunahitaji kutembea ndani yake. Lakini ni muhimu kuzijua, kuziamini ili tuweze kuziona zikidhirika maishani mwetu. Kila siku, kuna ahadi kwa ajili yako. Unapoanza siku yako, pata kufahamu ahadi hizi!
More
Tunataka kushukuru Joyce Meyer Ministries kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: tv.joycemeyer.org/kiswahili