Ahadi za kila siku ya maisha yakoMfano
Njia 6 za kufanya mazoezi ya amani
Kuishi katika amani ya Mungu ni muhimu katika kufurahia maisha. Ninaamini kwamba moja ya funguo za kuishi na amani katika maisha yako ni kuchukua hatua ndogo kuelekea amani kila siku. Hapa kuna vidokezo vichache ambavyo unaweza kutumia ili kuendeleza maisha ya amani zaidi.
- Chagua jinsi unavyotumia muda wako. Unaweza kuwa unajaribu kufanya vitu vingi sana na kutomaliza hata kimoja. Haraka ni hali ya mwili kujaribu kufanya zaidi kuliko Roho Mtakatifu anayekuongoza kufanya. Ongozwa na Roho.
- Kuwa tayari kusema "hapana" kwa urahisi. Wakati mwingine tunachukua vitu ambavyo hatupaswi kwa sababu hatuwezi kusema hapana. Mwambie Mungu akupe maneno ya kusema hapana wakati unafaa kukataa
- Pinga roho ya kuchelewa kufanya mambo. Neno la Mungu linatuambia tuwe na nidhamu. Fanya kile unachojua unahitaji kufanya sasa ili uweze kufurahia kikamilifu nyakati zako za kupumzika.
- Ondoa vikwazo muhimu. Ikiwa unajua unakabiliwa na vikwazo fulani, kama vile kutazama televisheni, weka miongozo yako mwenyewe.
- Weka mipaka inayofaa kwa usumbufu wowote ule. Maisha yamejaa vurugu, lakini unaweza kujifunza kuweka mipaka ambayo inakusaidia kushugulika nayo kwa njia njema, kama vile ratiba ya wakati unapoweka "mipaka."
- Badilisha maisha yako. Uliza Mungu akuonyeshe njia mbadala ili kuokoa muda na shida. Kwa mfano, wakati sina muda wa kuosha sahani, ninatumia sahani za karatasi!
Cha msingi ni kufanya amani kipaumbele, kuchukua hatua za vitendo kuelekea hilo, na umruhusu Mungu akuongoze kila siku katika amani yake kamilifu.
OMBI LA KUANZA SIKU
Mungu, nielekeze kwenye amani Yako ambayo hupita ufahamu wote. Nionyeshe hatua za kila siku ambazo ninaweza kuchukua ili kutembea katika amani yako kwa ajili yangu.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Mungu ametupa ahadi tele ambazo tunahitaji kutembea ndani yake. Lakini ni muhimu kuzijua, kuziamini ili tuweze kuziona zikidhirika maishani mwetu. Kila siku, kuna ahadi kwa ajili yako. Unapoanza siku yako, pata kufahamu ahadi hizi!
More
Tunataka kushukuru Joyce Meyer Ministries kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: tv.joycemeyer.org/kiswahili