Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Ahadi za kila siku ya maisha yakoMfano

Ahadi za kila siku ya maisha yako

SIKU 29 YA 30

Angalia kutoka mahali ulipo

Inaonekana kwamba maisha daima   ina njia zake za kutuleta mahali ambapo tunahitaji kuwa na mwanzo mpya.
Katika Biblia, Abramu alijikuta   mahali hapo wakati Loti mpwa wake alichagua ardhi bora zaidi katika eneo   hilo, akiwaacha Abramu na nchi isiyofaa sana. Lakini Mungu hakumuacha Abramu.   Badala yake alitokea na akampa Abramu maono mapya.

Ninapenda kile   Bwana alimwambia Abramu baada ya yeye na Loti kutengana. Akamwambia, " Inua sasa   macho yako, ukatazame kutoka hapo ulipo.."
Ni maneno hayo, “angalia kutoka   mahali ulipo”, ambayo ninasisitiza. Hiyo ni hatua ya mwanzo mpya ... kuanza upya.   Mungu mwenyewe atatuleta kwa wakati huo mara kwa mara.
Unaweza kuwa katika wakati huo   sasa. Labda unataka kuvunja tabia mbaya au kufufua ndoto iliyopotea. Labda   unataka kushughulikia juu ya fedha zako, kuanza biashara yako mwenyewe,   kuandika kitabu ... chochote kile, na Mungu anaweza kukuambia uanze sasa. Hii   inaweza kuwa mwanzo wako mpya!

Baada ya Mungu   kumwambia Abramu kuangalia kutoka mahali hapo, jambo lile alimwambia   lilikuwa, "Simama, tembea katika   nchi kwa urefu wake na upana wake, kwa maana nimekupa" (Mwanzo   13:17).
Mungu anaweza kukuambia sasa   hivi uamke na kuendelea na ndoto yako au maono ... kazi yako ... maisha yako,   kwa sababu Yeye amekupa. Sehemu yako ni kuendelea kutembea

Fanya kile   unachohitaji kufanya. Inaweza kuwa si rahisi. Inaweza kuchukua muda. Lakini mwamini   Mungu na uendelee kufanya kile unachohitaji kutenda

. Angalia   mahali ulipo sasa-na uendelee mbele!

OMBI LA KUANZA SIKU

Mungu, bila   kujali kilichotokea katika siku za nyuma, nisaidie kuangalia juu kutoka hapa   nilipo. Ninakushukuru kwa mwanzo wako mpya kwa ajili yangu. Mimi nitaingia   kwa ujasiri ndani yake na kutembea kwa ujasiri sawia na wito wako kwa ajili   yangu.

Andiko

siku 28siku 30

Kuhusu Mpango huu

Ahadi za kila siku ya maisha yako

Mungu ametupa ahadi tele ambazo tunahitaji kutembea ndani yake. Lakini ni muhimu kuzijua, kuziamini ili tuweze kuziona zikidhirika maishani mwetu. Kila siku, kuna ahadi kwa ajili yako. Unapoanza siku yako, pata kufahamu ahadi hizi! 

More

Tunataka kushukuru Joyce Meyer Ministries kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: tv.joycemeyer.org/kiswahili