Ahadi za kila siku ya maisha yakoMfano
Shiriki injili kwa kukutana na mahitaji ya watu
Niliwahi kusikia hadithi kuhusu mhubiri huko Urusi ambaye alikuwa akitembea akizungumza na watu, "Yesu anakupenda. Yesu anakupenda. "Alikuwa akitoa vijikaratasi vya Injili, na mwanamke mmoja akasema," Unajua nini? Njia yako ya mahubiri na Injili haijaza tumbo langu. "
Hadithi hii ina ujumbe muhimu: Wakati mwingine tunahitaji kuonyesha watu upendo wa Mungu kwa kukutana na mahitaji yao ya kimwili na kisha tunaweza kushiriki Injili ya Kristo.
Yesu alizungumzia umuhimu wa kukutana na mahitaji ya kimwili ya watu. Katika Mathayo 25, alisema kuwa tunapowapa wenye njaa chakula, au kutoa maji kwa walio na kiu, au kuvalisha maskini, au kuwajali wagonjwa, ni kama tunafanya mambo hayo kwa ajili yake. Alituonyesha jinsi kumsaidia mtu kwa njia ya vitendo kunaweza kujenga fursa nzuri ya kushiriki Injili na mtu.
Wakati mtu anaweza kuona upendo wa Mungu kwa vitendo kwa njia halisi katika maisha yao, ni rahisi sana kwao kuamini ujumbe wetu kwamba Mungu anawapenda.
Kwa hiyo inaonekanaje kihalisia? Inaweza kuanza na kitu kidogo, kama kumkumbatia mtu aliye karibu nawe anayehisi kuwa hapendeki. Baada ya hayo, unaweza kuendelea kuunga mkono huduma zinazosaidia wagonjwa, wenye kiu na wenye njaa. Labda unaweza kujitolea kupika au kuwafikia watu katika eneo lako au kuchukua safari ya ujumbe ili kuwahudumia wale wanaohitaji katika nchi nyingine.
Kuna uwezekano mwingi wakati unapofanya uamuzi wa kutumikia wengine sio kwa maneno tu, bali pia kupitia hatua za vitendo.
OMBI LA KUANZA SIKU
Bwana, nataka kuweka hatua nyuma ya maneno yangu. Nionyeshe jinsi ninavyoweza kuwasaidia watu unaowaletea njia yangu ili waweze kuhisi nguvu za upendo wako
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Mungu ametupa ahadi tele ambazo tunahitaji kutembea ndani yake. Lakini ni muhimu kuzijua, kuziamini ili tuweze kuziona zikidhirika maishani mwetu. Kila siku, kuna ahadi kwa ajili yako. Unapoanza siku yako, pata kufahamu ahadi hizi!
More
Tunataka kushukuru Joyce Meyer Ministries kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: tv.joycemeyer.org/kiswahili