Ahadi za kila siku ya maisha yakoMfano
Kupata amani ya Mungu kwa kuishi katika sasa
Kuwa na mtazamo wa utulivu na wa amani ni wa thamani sana. Ni mtazamo unaosema, "Ninaamini Mungu," na inaongea kwa nguvu kwa watu. Lakini inachukua muda, kuzingatia, na neema ya Mungu kuwa na amani wakati wote.
Mara nyingi kiwango cha shida yetu kimefungwa katika mazingira yetu. Unaweza kupata msongo wa akili kwa sababu unashughulika daima au unajitahidi kifedha au kwa sababu hauelewani na mtu unayempenda.
Ili kushinda msongo wa akili katika maisha yetu, tunahitaji kujifunza kuenenda katika amani ambayo imetolewa kwetu kwa nguvu ya kushinda ya Yesu.
Njia moja ya kuendeleza amani thabiti ni kujifunza kuishi "sasa." Tunaweza kutumia muda mwingi kufikiri juu ya siku za nyuma au kujiuliza nini kitatukia siku za mbeleni ... lakini hatuwezi kuafikia chochote isipokuwa akili zetu zimezingatia leo.
Biblia inatuambia kwamba Mungu anatupa neema kwa kila siku tunayoishi. Ninaamini neema ya Mungu ni nguvu inayowezesha na kutuwezesha kufanya kile tunachohitaji kufanya-na Yeye hutoa kwa ukarimu, kama tunavyohitaji.
Kila siku tunahitaji kusema, "Mungu amenipa leo. Nitafurahi na kushangalia ndani yake. "
Ikiwa unaweza kujifunza kumwamini Mungu "kwa sasa," na kupokea neema Yake kama unavyohitaji, unaweza kuwa mtu mwenye amani kweli-na hiyo ni nguvu.
OMBI LA KUANZA SIKU
Mungu, najua kwamba umeshinda kikwazo chochote, kwa hiyo nakuuliza Unisaidie kuishi katika amani ambayo umenipa. Nionyeshe jinsi ya kukuamini Wewe kama ninaishi katika"sasa."
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Mungu ametupa ahadi tele ambazo tunahitaji kutembea ndani yake. Lakini ni muhimu kuzijua, kuziamini ili tuweze kuziona zikidhirika maishani mwetu. Kila siku, kuna ahadi kwa ajili yako. Unapoanza siku yako, pata kufahamu ahadi hizi!
More
Tunataka kushukuru Joyce Meyer Ministries kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: tv.joycemeyer.org/kiswahili