Oswald Chambers: Furaha- Nguvu katika BwanaMfano
Hata ikiwa wewe ni mwerevu ama mjinga, mtakatifu au la, mfalme ama aliyedhulumiwa na mfalme, aliyefuzu au aliyefeli, katika jamii au peke yako, mwenye kichwa ngumu au mjanja, wote wana hatima mmoja. Yote yanapita, Solomoni anasema, na hatuwezi kupata furaha unaodumu katika kitu chochote ambacho tunapenda kugusa. Mja akijaribu kupata furaha ya kweli katika semi lolote la ukweli, ama kutimizika kwa ndoto, ama upweke kimwili au kifikra, ama katika jamii ni balaa; atapata furaha kwa uhusiano wa kibinafsi na Yesu Kristo pekee. Yesu Kristu ni Mungu akidhihirika katika binadamu, na lazima tupuuze hata mpaka kuchukia chochote ambacho kinashandana na uhusiano wetu naye.
Furaha ya kweli ya maisha ya mtu ni katika uhusiano wake na Mungu, na kidokezo kikuu cha uhakikisho wa Mhebrania katika Mungu ni kuwa Mungu haondoi ufaafu wa mtu kwa maisha yake. Hili ndilo daima jaribio la dini bandia.
Maswali ya Kutafakari: Nimetafuta furaha wapi? Nimetarajia kupata furaha katika tamaa zipi, imani ipi, ama dhamira zipi? Nimetafuta furaha katika mahusiano yapi ya watu?
Dondoo imetoka "Still Higher for His Highest", © Discovery House Publishers

Andiko
Kuhusu Mpango huu
Gundua hekima ya Oswald Chambers, mwandishi wa "My Utmost for His Highest", katika mkusanyiko huu wa hazina ambao unatoa ufahamu kuhusu furaha. Kila somo lina dondoo kutoka Chambers na maswali ya kutafakari kibinafsi. Akitumia hekima sahili na dhahiri kutoka Biblia kukupa motisha na changamoto, utaanza kutamani kuwasiliana zaidi na Mungu.
More
We would like to thank Discovery House Publishers for providing this plan. For more information, please visit: www.utmost.org