Oswald Chambers: Furaha- Nguvu katika BwanaMfano
Kila kitu ambacho kimefichika au hakijulikani wakati huu utakuwa waziri siku moja, wazi kama vitu tunavyoona wakati huu, uwazi unaong'aa na wenye furaha. Ndio maana Mungu anatuhimiza tuwe wenye subira. Haba na haba kila kitu kitafichuliwa mpaka tuelewe kama vile Yesu alivyoelewa. Mbinguni utakuwa wa kumjua na kumwelewa Mungu daima, na, tumshukuru Mungu, tunaweza kuanza kumjua Yesu hapa duniani. Maisha yaliyotakaswa yana maana kwamba tunaanza kumwelewa Mungu na kudhihirisha maisha ya Mwana wa Mungu katika mwili huu tunao ambao utakufa.
Kila ujuzi tunao kuhusu Mungu inatupa furaha isiyo kifani. Tukimwelewa Mungu katika jambo moja tutaelewa kidogo furaha ambayo Yesu alikuwa nayo. Ni milki njema, ni hulka yenyewe ya Yesu.
Maswali ya Kutafakari: Ninafurahia ufunuo wa Mungu ambao unachukua muda kufunuliwa ama ninaudhika kwa sababu Mungu hana haraka? Ikiwa Mungu haharakishi, mbona ninaharakisha? Nitafurahia ujuzi vipi ikiwa sifurahii ugunduzi?
Dondoo imetoka "Our Brilliant Heritage", © Discovery House Publishers

Andiko
Kuhusu Mpango huu
Gundua hekima ya Oswald Chambers, mwandishi wa "My Utmost for His Highest", katika mkusanyiko huu wa hazina ambao unatoa ufahamu kuhusu furaha. Kila somo lina dondoo kutoka Chambers na maswali ya kutafakari kibinafsi. Akitumia hekima sahili na dhahiri kutoka Biblia kukupa motisha na changamoto, utaanza kutamani kuwasiliana zaidi na Mungu.
More
We would like to thank Discovery House Publishers for providing this plan. For more information, please visit: www.utmost.org