Oswald Chambers: Furaha- Nguvu katika BwanaMfano
Hebu fikiri kama Bwana wetu angepima maisha yake kwa kuona ikiwa aliwabariki watu au la. Alikuwa “kikwazo” kwa wengi, kwa majirani wake, kwa taifa lake, kwa sababu kupitia kwake walikufuru Roho Mtakatifu, na nchini mwake “Haku[do] miujiza mingi pale kwa sababu ya kutoamini kwao” (Mathayo 13:58).
Ikiwa Bwana Wetu angepima maisha yake kwa matokeo yaliyodhihirika wazi, angehuzunika mno. Hatupo hapa kufanya watu waokoke, kutenda wema kwa wengine; haya ni matokeo yanayotarajiwa, lakini si nia yetu, na hapa ndipo wengi wetu wanaacha kuwa wafuasi. Tutamfuata Mungu ikiwa atatufanya tuwe baraka kwa wengine, lakini asipofanya hivyo hatutamfuata. Furaha ya kitu chochote, kwa mfano unyasi unaokua, ni kutimiza lengo la kuumbwa kwake—kwamba kisifu utukufu wa Mungu.
Maswali ya Kutafakari: Ninatumia kipimo kipi kupima maisha yangu? Ninatumia vipimo vya Mungu kama vile uaminifu na ucha Mungu ama natumia vipimo vya ulimwengu kama vile umaarufu, tija na ufanisi?
Dondoo imetoka "The Love of God", © Discovery House Publishers

Andiko
Kuhusu Mpango huu
Gundua hekima ya Oswald Chambers, mwandishi wa "My Utmost for His Highest", katika mkusanyiko huu wa hazina ambao unatoa ufahamu kuhusu furaha. Kila somo lina dondoo kutoka Chambers na maswali ya kutafakari kibinafsi. Akitumia hekima sahili na dhahiri kutoka Biblia kukupa motisha na changamoto, utaanza kutamani kuwasiliana zaidi na Mungu.
More
We would like to thank Discovery House Publishers for providing this plan. For more information, please visit: www.utmost.org