Oswald Chambers: Furaha- Nguvu katika BwanaMfano
Ikiwa hali yako ni ngumu wakati huu, kumbuka wakati ambao haikuwa ngumu, na utashangaa jinsi moyo wa mwanadamu una uwezo wa kujirudisha na kugeuka kutoka kitu kimoja hadi kingine. Moyo wa mwanadamu unaweza kuvumilia huzuni mwingi, na vilevile furaha mpwitompwito! Ikiwa tutapoteza uwezo wa kugeuka kutoka kimoja hadi kingine, tunaharibu uwiano. Roho ya Mungu inarudisha na kuendeleza uwiano unaofaa.
Kuhubiri injili ya “changamka,” ingawa mtu hawezi kuchangamka. Kumwambia atazamie upande bora wa maisha ihali hakuna upande mzuri ni ujinga kama kumwambia samaki atazame mchezo wa kuigiza wa Handel. Vilevile utaambulia patupu ukimwambia mtu aliyeelewa kwamba ametenda dhambi achangamke. Anachohitaji ni neema ya Mungu kumbadilisha na kumweka katika chemchemi ya furaha.
Maswali ya Kutafakari: Ninaridhishwa na uchangamfu au furaha? Uhakikisho wetu katika Mungu yanatosha kutupa furaha hata katika msimu wa huzuni? Tajriba gani ni mkuu kwangu: neema ama dhambi zangu?
Dondoo imetoka "Biblical Psychology", © Discovery House Publishers

Andiko
Kuhusu Mpango huu
Gundua hekima ya Oswald Chambers, mwandishi wa "My Utmost for His Highest", katika mkusanyiko huu wa hazina ambao unatoa ufahamu kuhusu furaha. Kila somo lina dondoo kutoka Chambers na maswali ya kutafakari kibinafsi. Akitumia hekima sahili na dhahiri kutoka Biblia kukupa motisha na changamoto, utaanza kutamani kuwasiliana zaidi na Mungu.
More
We would like to thank Discovery House Publishers for providing this plan. For more information, please visit: www.utmost.org