Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Zaburi 72:1-11

Zaburi 72:1-11 BHN

Ee Mungu, umjalie mfalme uamuzi wako, umpe mwanamfalme uadilifu wako; atawale taifa lako kwa haki, na maskini wako kwa uadilifu. Milima ilete fanaka kwa watu wako, vilima vijae uadilifu. Mfalme awatetee wanyonge wa taifa, awasaidie watoto wa fukara, na kuwaangamiza watu wadhalimu. Mfalme aishi muda mrefu kama jua, na kama mwezi, kwa vizazi vyote. Awe kama manyunyu yaburudishayo mashamba, kama mvua iinyweshayo ardhi. Uadilifu ustawi maisha yake yote, na amani kwa wingi mpaka mwezi ukome. Atawale kutoka bahari hata bahari, kutoka mto Eufrate hata mipaka ya dunia. Maadui zake wakaao nyikani wanyenyekee mbele yake, washindani wake walambe vumbi. Wafalme wa Tarshishi na visiwa wamlipe kodi, wafalme wa Sheba na Seba wamletee zawadi. Wafalme wote wa dunia wamheshimu, watu wa mataifa yote wamtumikie.

Soma Zaburi 72