Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Zaburi 72:1-11

Zaburi 72:1-11 SRUV

Ee Mungu, mpe mfalme hukumu zako, Na mwana wa mfalme haki yako. Atawaamua watu wako kwa haki, Na watu wako walioonewa kwa hukumu. Milimana iwaletee watu amani, Na pamoja na vilima, ilete haki. Na atawatetea watu walioonewa, Awaokoe wahitaji, na kumwaangamiza mdhalimu. Watakuogopa wakati wote wa kudumu jua, Na wakati wa kung'aa mwezi kizazi hata kizazi. Atashuka kama mvua juu ya majani yaliyokatwa, Kama manyunyu yainyweshayo nchi. Haki na isitawi wakati wa maisha yake yote, Nayo amani iwepo, hadi mwezi utakapokoma. Na awe na enzi toka bahari hadi bahari, Toka Mto hadi miisho ya dunia. Wakaao jangwani na wainame mbele zake; Adui zake na warambe mavumbi. Wafalme wa Tarshishi na visiwa na walete kodi; Wafalme wa Sheba na Seba na watoe vipawa. Naam, wafalme wote na wamsujudie; Na mataifa yote wamtumikie.

Soma Zaburi 72