Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Zaburi 72

72
Sala ya kumtakia mfalme neema
Ya Sulemani
1Ee Mungu, mpe mfalme hukumu zako,
Na mwana wa mfalme haki yako.
2 # Isa 11:2 Atawaamua watu wako kwa haki,
Na watu wako walioonewa kwa hukumu.
3Milimana iwaletee watu amani,
Na pamoja na vilima, ilete haki.
4Na atawatetea watu walioonewa,
Awaokoe wahitaji, na kumwaangamiza mdhalimu.
5Watakuogopa wakati wote wa kudumu jua,
Na wakati wa kung'aa mwezi kizazi hata kizazi.
6 # 2 Sam 23:4; Hos 6:3 Atashuka kama mvua juu ya majani yaliyokatwa,
Kama manyunyu yainyweshayo nchi.
7 # Isa 2:4; Dan 2:44; Lk 1:33 Haki na isitawi wakati wa maisha yake yote,
Nayo amani iwepo, hadi mwezi utakapokoma.
8 # Kut 23:31; 1 Fal 4:21,24; Zab 2:8; Zek 9:10 Na awe na enzi toka bahari hadi bahari,
Toka Mto hadi miisho ya dunia.
9Wakaao jangwani na wainame mbele zake;
Adui zake na warambe mavumbi.
10 # Isa 49:7 Wafalme wa Tarshishi na visiwa na walete kodi;
Wafalme wa Sheba na Seba na watoe vipawa.
11Naam, wafalme wote na wamsujudie;
Na mataifa yote wamtumikie.
12Kwa maana atamkomboa mhitaji aliapo,
Na mtu aliyeonewa iwapo hana msaidizi.
13Atawahurumia wanyonge na maskini,
Na nafsi za wahitaji ataziokoa.
14Atawakomboa kutoka kwa maonevu na udhalimu,
Maana damu yao ina thamani machoni pake.
15 # Mt 6:10; 1 Kor 1:2,3 Na aishi maisha marefu!
Na wampe dhahabu ya Sheba;
Na wamwombee daima;
Na kumbariki mchana kutwa.
16 # 1 Fal 4:20 Na uwepo wingi wa nafaka
Katika ardhi juu ya milima;
Matunda yake na yawayewaye kama ilivyo katika milima ya Lebanoni,
Na watu wa mjini wasitawi kama majani ya nchi.
17 # Mwa 12:3; Yer 4:2; Isa 45:23,24; Lk 1:48; Flp 2:9-11 Jina lake na lidumu milele,
Pindi ling'aapo jua, umaarufu wake uwepo;
Mataifa yote na wabarikiwe katika yeye,
Na kumwita heri.
* * *
18Na ahimidiwe BWANA, Mungu, Mungu wa Israeli,
Atendaye miujiza Yeye peke yake;
19Jina lake tukufu na lihimidiwe milele;
Dunia yote na ijae utukufu wake. Amina na Amina.
* * *
20Maombi ya Daudi mwana wa Yese, yamekwisha.

Iliyochaguliwa sasa

Zaburi 72: SRUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia