Zab 72:1-11
Zab 72:1-11 SUV
Ee Mungu, mpe mfalme hukumu zako, Na mwana wa mfalme haki yako. Atawaamua watu wako kwa haki, Na watu wako walioonewa kwa hukumu. Milima itawazalia watu amani, Na vilima navyo kwa haki. Atawahukumu walioonewa wa watu, Atawaokoa wahitaji, atamseta mwenye kuonea. Watakuogopa wakati wote wa kudumu jua, Na wakati wa kung’aa mwezi kizazi hata kizazi. Atashuka kama mvua juu ya majani yaliyokatwa, Kama manyunyu yainyweshayo nchi. Siku zake yeye, mtu mwenye haki atasitawi, Na wingi wa amani hata mwezi utakapokoma. Na awe na enzi toka bahari hata bahari, Toka Mto hata miisho ya dunia. Wakaao jangwani na wainame mbele zake; Adui zake na warambe mavumbi. Wafalme wa Tarshishi na visiwa na walete kodi; Wafalme wa Sheba na Seba na watoe vipawa. Naam, wafalme wote na wamsujudie; Na mataifa yote wamtumikie.