Zaburi 72:1-11
Zaburi 72:1-11 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Ee Mungu, mpe mfalme hukumu zako, Na mwana wa mfalme haki yako. Atawaamua watu wako kwa haki, Na watu wako walioonewa kwa hukumu. Milimana iwaletee watu amani, Na pamoja na vilima, ilete haki. Na atawatetea watu walioonewa, Awaokoe wahitaji, na kumwaangamiza mdhalimu. Watakuogopa wakati wote wa kudumu jua, Na wakati wa kung'aa mwezi kizazi hata kizazi. Atashuka kama mvua juu ya majani yaliyokatwa, Kama manyunyu yainyweshayo nchi. Haki na isitawi wakati wa maisha yake yote, Nayo amani iwepo, hadi mwezi utakapokoma. Na awe na enzi toka bahari hadi bahari, Toka Mto hadi miisho ya dunia. Wakaao jangwani na wainame mbele zake; Adui zake na warambe mavumbi. Wafalme wa Tarshishi na visiwa na walete kodi; Wafalme wa Sheba na Seba na watoe vipawa. Naam, wafalme wote na wamsujudie; Na mataifa yote wamtumikie.
Zaburi 72:1-11 Biblia Habari Njema (BHN)
Ee Mungu, umjalie mfalme uamuzi wako, umpe mwanamfalme uadilifu wako; atawale taifa lako kwa haki, na maskini wako kwa uadilifu. Milima ilete fanaka kwa watu wako, vilima vijae uadilifu. Mfalme awatetee wanyonge wa taifa, awasaidie watoto wa fukara, na kuwaangamiza watu wadhalimu. Mfalme aishi muda mrefu kama jua, na kama mwezi, kwa vizazi vyote. Awe kama manyunyu yaburudishayo mashamba, kama mvua iinyweshayo ardhi. Uadilifu ustawi maisha yake yote, na amani kwa wingi mpaka mwezi ukome. Atawale kutoka bahari hata bahari, kutoka mto Eufrate hata mipaka ya dunia. Maadui zake wakaao nyikani wanyenyekee mbele yake, washindani wake walambe vumbi. Wafalme wa Tarshishi na visiwa wamlipe kodi, wafalme wa Sheba na Seba wamletee zawadi. Wafalme wote wa dunia wamheshimu, watu wa mataifa yote wamtumikie.
Zaburi 72:1-11 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Ee Mungu, mpe mfalme hukumu zako, Na mwana wa mfalme haki yako. Atawaamua watu wako kwa haki, Na watu wako walioonewa kwa hukumu. Milimana iwaletee watu amani, Na pamoja na vilima, ilete haki. Na atawatetea watu walioonewa, Awaokoe wahitaji, na kumwaangamiza mdhalimu. Watakuogopa wakati wote wa kudumu jua, Na wakati wa kung'aa mwezi kizazi hata kizazi. Atashuka kama mvua juu ya majani yaliyokatwa, Kama manyunyu yainyweshayo nchi. Haki na isitawi wakati wa maisha yake yote, Nayo amani iwepo, hadi mwezi utakapokoma. Na awe na enzi toka bahari hadi bahari, Toka Mto hadi miisho ya dunia. Wakaao jangwani na wainame mbele zake; Adui zake na warambe mavumbi. Wafalme wa Tarshishi na visiwa na walete kodi; Wafalme wa Sheba na Seba na watoe vipawa. Naam, wafalme wote na wamsujudie; Na mataifa yote wamtumikie.
Zaburi 72:1-11 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Ee Mungu, mpe mfalme hukumu zako, Na mwana wa mfalme haki yako. Atawaamua watu wako kwa haki, Na watu wako walioonewa kwa hukumu. Milima itawazalia watu amani, Na vilima navyo kwa haki. Atawahukumu walioonewa wa watu, Atawaokoa wahitaji, atamseta mwenye kuonea. Watakuogopa wakati wote wa kudumu jua, Na wakati wa kung’aa mwezi kizazi hata kizazi. Atashuka kama mvua juu ya majani yaliyokatwa, Kama manyunyu yainyweshayo nchi. Siku zake yeye, mtu mwenye haki atasitawi, Na wingi wa amani hata mwezi utakapokoma. Na awe na enzi toka bahari hata bahari, Toka Mto hata miisho ya dunia. Wakaao jangwani na wainame mbele zake; Adui zake na warambe mavumbi. Wafalme wa Tarshishi na visiwa na walete kodi; Wafalme wa Sheba na Seba na watoe vipawa. Naam, wafalme wote na wamsujudie; Na mataifa yote wamtumikie.
Zaburi 72:1-11 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Ee Mungu, mjalie mfalme aamue kwa haki yako, mwana wa mfalme kwa haki yako. Atawaamua watu wako kwa haki, watu wako walioonewa kwa haki. Milima italeta mafanikio kwa watu, vilima tunda la haki. Atawatetea walioonewa miongoni mwa watu na atawaokoa watoto wa wahitaji, ataponda mdhalimu. Atadumu kama jua lidumuvyo, kama mwezi, vizazi vyote. Atakuwa kama mvua inyeshayo juu ya shamba lililofyekwa, kama manyunyu yanyeshayo ardhi. Katika siku zake wenye haki watastawi; mafanikio yatakuwepo mpaka mwezi utakapokoma. Atatawala kutoka bahari hadi bahari na kutoka Mto mpaka miisho ya dunia. Makabila ya jangwani watamsujudia, na adui zake wataramba mavumbi. Wafalme wa Tarshishi na wa pwani za mbali watamletea kodi; wafalme wa Sheba na Seba watampa zawadi. Wafalme wote watamsujudia na mataifa yote yatamtumikia.