Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Zaburi 72:1-11

Zaburi 72:1-11 NENO

Ee Mungu, mjalie mfalme aamue kwa haki yako, mwana wa mfalme kwa haki yako. Atawaamua watu wako kwa haki, watu wako walioonewa kwa haki. Milima italeta mafanikio kwa watu, vilima tunda la haki. Atawatetea walioonewa miongoni mwa watu na atawaokoa watoto wa wahitaji, ataponda mdhalimu. Atadumu kama jua linavyodumu, kama mwezi, vizazi vyote. Atakuwa kama mvua inavyonyesha juu ya shamba lililofyekwa, kama manyunyu yanavyonyeshea ardhi. Katika siku zake wenye haki watastawi; mafanikio yatakuwepo hadi mwezi utakapokoma. Atatawala kutoka bahari hadi bahari na kutoka Mto hadi miisho ya dunia. Makabila ya jangwani watamsujudia, na adui zake wataramba mavumbi. Wafalme wa Tarshishi na wa pwani za mbali watamletea ushuru; wafalme wa Sheba na Seba watampa zawadi. Wafalme wote watamsujudia na mataifa yote yatamtumikia.