Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Zaburi 104:24-30

Zaburi 104:24-30 BHN

Ee Mwenyezi-Mungu, umetenda mambo mengi mno! Yote umeyafanya kwa hekima! Dunia imejaa viumbe vyako! Mbali kule iko bahari - kubwa na pana, ambamo kumejaa viumbe visivyohesabika, viumbe hai, vikubwa na vidogo. Ndimo zinamosafiri meli, na lile dude Lewiyathani uliloliumba licheze humo. Wote wanakungojea wewe, uwapatie chakula chao kwa wakati wake. Wanaokota chochote kile unachowapa; ukifumbua mkono wako wanashiba vinono. Ukiwapa kisogo, wanaogopa; ukiondoa pumzi yao, wanakufa, na kurudi mavumbini walimotoka. Ukiwapulizia pumzi yako, wanaishi tena; wewe waipa dunia sura mpya.

Soma Zaburi 104

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha