Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Zaburi 104:24-30

Zaburi 104:24-30 SRUV

Ee BWANA, jinsi yalivyo mengi matendo yako! Kwa hekima umevifanya vyote pia. Dunia imejaa viumbe wako. Bahari iko kule, kubwa na upana, Ndimo mlimo viendavyo visivyohesabika, Viumbe hai wakubwa kwa wadogo. Ndimo zipitamo merikebu, Ndimo alimo Lewiathani uliyemwumba acheze humo. Hao wote wanakungoja Wewe, Uwape chakula chao kwa wakati wake. Wewe huwapa, Wao wanakiokota; Wewe waukunjua mkono wako, Wao wanashiba mema; Wewe wauficha uso wako, Wao wanafadhaika; Waiondoa pumzi yao, wanakufa, Na kuyarudia mavumbi yao, Waituma roho yako, wanaumbwa, Nawe waufanya upya uso wa nchi.

Soma Zaburi 104

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha