Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Zab 104:24-30

Zab 104:24-30 SUV

Ee BWANA, jinsi yalivyo mengi matendo yako! Kwa hekima umevifanya vyote pia. Dunia imejaa mali zako. Bahari iko kule, kubwa na upana, Ndimo mlimo viendavyo visivyohesabika, Viumbe hai vidogo kwa vikubwa. Ndimo zipitamo merikebu, Ndimo alimo lewiathani uliyemwumba acheze humo. Hao wote wanakungoja Wewe, Uwape chakula chao kwa wakati wake. Wewe huwapa, Wao wanakiokota; Wewe waukunjua mkono wako, Wao wanashiba mema; Wewe wauficha uso wako, Wao wanafadhaika; Waiondoa pumzi yao, wanakufa, Na kuyarudia mavumbi yao, Waipeleka roho yako, wanaumbwa, Nawe waufanya upya uso wa nchi.

Soma Zab 104

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha