Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Zaburi 104:24-30

Zaburi 104:24-30 NEN

Ee BWANA, jinsi matendo yako yalivyo mengi! Kwa hekima ulizifanya zote, dunia imejaa viumbe vyako. Pale kuna bahari, kubwa na yenye nafasi tele, imejaa viumbe visivyo na idadi, vitu vyenye uhai vikubwa na vidogo. Huko meli huenda na kurudi, pia Lewiathani, uliyemuumba acheze ndani yake. Hawa wote wanakutazamia wewe, uwape chakula chao kwa wakati wake. Wakati unapowapa, wanakikusanya, unapofumbua mkono wako, wao wanashibishwa mema. Unapoficha uso wako, wanapata hofu, unapoondoa pumzi yao, wanakufa na kurudi mavumbini. Unapopeleka Roho wako, wanaumbwa, nawe huufanya upya uso wa dunia.

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha