Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Ayubu 27:13-23

Ayubu 27:13-23 SRUV

Hii ndiyo sehemu ya mtu mwovu kwa Mungu, Na urithi wa hao waoneao, waupokeao kwa Mwenyezi. Watoto wake wakiongezeka ni kwa upanga; Na wazao wake hawatashiba chakula. Hao watakaosalia kwake watakufa kwa maradhi mabaya, Wala wajane wake waliofiwa na waume hawataomboleza. Ajapokusanya fedha kama mavumbi, Na kujifanyia mavazi kama udongo kwa wingi; Yumkini kuyatengeza, lakini wenye haki watayavaa, Nao wasio na hatia watazigawanya hizo fedha. Yeye hujenga nyumba yake kama mdudu, Na kama kibanda afanyacho mlinzi. Yeye hujilaza hali ni tajiri, lakini ndio mwisho; Hufunua macho yake, naye hayuko. Vitisho vyampata kama maji mengi; Dhoruba humwiba usiku. Upepo wa mashariki humchukua, naye huondoka; Na kumkumba atoke mahali pake. Kwani Mungu atamtupia asimhurumie; Angependa kuukimbia mkono wake. Watu watampigia makofi, Na kumzomea atoke mahali pake.

Soma Ayubu 27