Yobu 27:13-23
Yobu 27:13-23 Biblia Habari Njema (BHN)
“Hiki ndicho Mungu alichomwekea mtu mwovu, alichopangiwa mdhalimu kupata ni hiki: Watoto wake hata wawe wengi watauawa kwa upanga; wazawa wake hawatakuwa na chakula cha kutosha. Wale watakaopona watakufa kwa maradhi mabaya, na wajane wao hawatawaombolezea. Hata akirundika fedha kama mavumbi, na mavazi kama udongo wa mfinyanzi, na arundike tu, lakini mnyofu ndiye atakayeyavaa, na fedha yake watagawana watu wasio na hatia. Nyumba ajengayo mwovu ni kama utando wa buibui, ni kama kibanda cha mlinzi shambani. Huenda kulala tajiri, lakini ni mara ya mwisho; atafungua macho yake, na utajiri wake umetoweka! Vitisho humvamia kama mafuriko; usiku hukumbwa na kimbunga. Upepo wa mashariki humpeperusha akatoweka; humfagilia mbali kutoka makao yake. Upepo huo humvamia bila huruma; atajaribu kuukimbia lakini mbio za bure. Upepo humzomea akimbiapo, na kumfyonya toka mahali pake.
Yobu 27:13-23 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Hii ndiyo sehemu ya mtu mwovu kwa Mungu, Na urithi wa hao waoneao, waupokeao kwa Mwenyezi. Watoto wake wakiongezeka ni kwa upanga; Na wazao wake hawatashiba chakula. Hao watakaosalia kwake watazikwa katika kufa, Wala wajane wake waliofiwa na waume hawataomboleza. Ajapokusanya fedha kama mavumbi, Na kujifanyia mavazi kama udongo kwa wingi; Yumkini kuyatengeza, lakini wenye haki watayavaa, Nao wasio na hatia watazigawanya hizo fedha. Yeye hujenga nyumba yake kama mdudu, Na kama kibanda afanyacho mlinzi. Yeye hujilaza hali ni tajiri, lakini ndio mwisho; Hufunua macho yake, naye hayuko. Vitisho vyampata kama maji mengi; Dhoruba humwiba usiku. Upepo wa mashariki humchukua, naye huondoka; Na kumkumba atoke mahali pake. Kwani Mungu atamtupia asimhurumie; Angependa kuukimbia mkono wake. Watu watampigia makofi, Na kumzomea atoke mahali pake.
Yobu 27:13-23 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Hii ndiyo sehemu ya mtu mwovu kwa Mungu, Na urithi wa hao waoneao, waupokeao kwa Mwenyezi. Watoto wake wakiongezeka ni kwa upanga; Na wazao wake hawatashiba chakula. Hao watakaosalia kwake watakufa kwa maradhi mabaya, Wala wajane wake waliofiwa na waume hawataomboleza. Ajapokusanya fedha kama mavumbi, Na kujifanyia mavazi kama udongo kwa wingi; Yumkini kuyatengeza, lakini wenye haki watayavaa, Nao wasio na hatia watazigawanya hizo fedha. Yeye hujenga nyumba yake kama mdudu, Na kama kibanda afanyacho mlinzi. Yeye hujilaza hali ni tajiri, lakini ndio mwisho; Hufunua macho yake, naye hayuko. Vitisho vyampata kama maji mengi; Dhoruba humwiba usiku. Upepo wa mashariki humchukua, naye huondoka; Na kumkumba atoke mahali pake. Kwani Mungu atamtupia asimhurumie; Angependa kuukimbia mkono wake. Watu watampigia makofi, Na kumzomea atoke mahali pake.
Yobu 27:13-23 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
“Hili ndilo fungu ambalo Mungu humpa mtu mwovu, urithi ule mtu mdhalimu anapokea kutoka kwa Mwenyezi: Hata kama watoto wake watakuwa wengi kiasi gani, fungu lao ni kuuawa kwa upanga; wazao wake hawatakuwa kamwe na chakula cha kuwatosha. Tauni itawazika wale watakaonusurika miongoni mwao, nao wajane wao hawatawaombolezea. Ajapokusanya fedha nyingi kama mavumbi, na mavazi kama malundo ya udongo wa mfinyanzi, yale yote mtu mwovu aliyojiwekea akiba, mwenye haki atayavaa, naye asiye na hatia ataigawanya fedha yake. Nyumba aijengayo ni kama utando wa buibui, kama kibanda alichotengeneza mlinzi. Yeye hulala akiwa tajiri, lakini ndiyo mara ya mwisho; afunguapo macho yake, yote yametoweka. Vitisho humjia kama mafuriko; dhoruba humkumba ghafula usiku. Upepo mkali wa mashariki humchukua, naye hutoweka; humzoa kutoka mahali pake. Humvurumisha bila huruma, huku akikimbia kasi kukwepa nguvu zake. Upepo humpigia makofi kwa dharau, na kumfukuza atoke mahali pake.