Ayubu 27
27
Ayubu ashikilia uelekevu wake
1Kisha Ayubu akaendelea na hoja yake, na kusema,
2 #
Ayu 34:5
Kama aishivyo Mungu, aliyeniondolea haki yangu;
Huyo Mwenyezi aliyeitesa nafsi yangu;
3(Kwa kuwa uhai wangu ungali mzima ndani yangu,
Na Roho ya Mungu iko katika pua yangu;)
4Hakika midomo yangu haitanena yasiyo haki,
Wala ulimi wangu hautatamka udanganyifu.
5 #
Ayu 13:15
Hasha! Nisiwahesabie ninyi kuwa na haki;
Hata nitakapokufa sitajiondolea uelekevu wangu.
6 #
Ayu 2:3; Mdo 24:16 Haki yangu naishika sana, wala sitaiacha;
Moyo wangu hautanisuta wakati nikiwapo hai.
7Adui yangu na awe kama huyo mwovu,
Na mpinzani wangu awe kama asiye haki.
8 #
Mt 16:26
Maana tumaini la mpotovu ni nini, ingawa ajipatia faida,
Hapo Mungu amwondoleapo roho yake?
9 #
Mit 1:28; Isa 1:15; Mik 3:4; Zek 7:13; Yak 4:3 Je! Mungu atakisikia kilio chake,
Taabu zitakapomfikia?
10 #
Ayu 22:26
Je! Atajifurahisha katika Mwenyezi,
Na kumlingana Mungu nyakati zote?
11Nitawafundisha ninyi mambo ya mkono wa Mungu;
Hayo yaliyo kwa Mwenyezi sitayaficha.
12Tazama, ninyi nyote mmeyaona wenyewe;
Mbona basi mmebatilika kabisa?
13Hii ndiyo sehemu ya mtu mwovu kwa Mungu,
Na urithi wa hao waoneao, waupokeao kwa Mwenyezi.
14 #
Kum 28:32,41; Est 9:10; 2 Fal 10:6-10 Watoto wake wakiongezeka ni kwa upanga;
Na wazao wake hawatashiba chakula.
15 #
Zab 78:64
Hao watakaosalia kwake watakufa kwa maradhi mabaya,
Wala wajane wake waliofiwa na waume hawataomboleza.
16Ajapokusanya fedha kama mavumbi,
Na kujifanyia mavazi kama udongo kwa wingi;
17 #
Mit 28:8; Mhu 2:26 Yumkini kuyatengeza, lakini wenye haki watayavaa,
Nao wasio na hatia watazigawanya hizo fedha.
18 #
Omb 2:6
Yeye hujenga nyumba yake kama mdudu,
Na kama kibanda afanyacho mlinzi.
19 #
Hes 20:26
Yeye hujilaza hali ni tajiri, lakini ndio mwisho;
Hufunua macho yake, naye hayuko.
20Vitisho vyampata kama maji mengi;
Dhoruba humwiba usiku.
21Upepo wa mashariki humchukua, naye huondoka;
Na kumkumba atoke mahali pake.
22Kwani Mungu atamtupia asimhurumie;
Angependa kuukimbia mkono wake.
23Watu watampigia makofi,
Na kumzomea atoke mahali pake.
Iliyochaguliwa sasa
Ayubu 27: SRUV
Kuonyesha
Shirikisha
Nakili
Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia
Swahili Revised Union Version Bible © Bible Society of Kenya, and Bible Society of Tanzania, 2005.