YouVersion Logo
Search Icon

BibleProject | Tafakari ya Ujio wa YesuSample

 BibleProject | Tafakari ya Ujio wa Yesu

DAY 3 OF 28

Kuwa na mtazamo chanya huchagua kuona jinsi hali zinavyoweza kuwa na matokeo bora. Tumaini la Biblia, hata hivyo, halitegemei hali. Tena, watu wenye matumaini katika Biblia mara nyingi hukabili nyakati ngumu bila ushahidi wowote kuwa mambo yatakuwa mepesi, lakini bado huchagua kuwa na tumaini. Kwa mfano, nabii wa Israeli Mika aliishi katikati ya ukosefu wa haki na uovu lakini alimtazamia Mungu kwa tumaini.

Soma: 

Mika 7:6-8 

Tafakari:

Angalia baadhi ya matatizo anayoorodhesha Mika katika mstari wa 6 na jinsi anavyojibu katika mstari wa 7 na 8. Baadhi ya matatizo yanayokuzunguka sasa hivi ni yapi? Jibu la Mika linakutia moyo au kukupatia changamoto vipi leo?

Chukua muda ili kurudia ombi la Mika kwa Mungu kwa maneno yako mwenyewe. Anakusikia.

Scripture

Day 2Day 4

About this Plan

 BibleProject | Tafakari ya Ujio wa Yesu

BibleProject ilibuni Tafakari ya Ujio wa Yesu ili kuhamasisha watu mmoja mmoja, vikundi vidogo vidogo, na familia kusherehekea majilio, au kuwasili kwa Yesu. Mwongozo huu wa wiki nne unashirikisha video za kikatuni, mihutasari mifupi, na maswali ya kutafakari ili kuwasaidia washiriki kuchunguza maana ya Biblia ya tumaini, amani, furaha, na upendo. Chagua mwongozo huu ili kujifunza jinsi maadili haya manne yamefika ulimwenguni kupitia kwa Yesu.

More