BibleProject | Tafakari ya Ujio wa YesuSample
Tumaini la Biblia hutegemea tabia ya Mungu kama msingi wa kuamini kuwa siku zijazo zitakuwa bora kuliko za sasa. Kadri mtu anavyoijua tabia ya Mungu kwa undani, ndivyo tumaini la huyo mtu linavyozidi kuongezeka.
Soma:
Zaburi 130:1-8
Tafakari:
Mtunzi wa zaburi anasema nini kuhusu tabia ya Mungu?
Unasema nini kuhusu tabia ya Mungu?
Mtunzi wa zaburi anaamini Mungu ataifanyia Israeli nini?
Unaamini Mungu atakufanyia wewe na jumuiya yako nini?
Je, unataka kuonaje upendo wa Mungu unaosamehe ukifanya kazi katika maisha yako na jumuiya yako wiki hii? Fanya jibu lako kuwa ombi kwake sasa. Anasikiliza.
Scripture
About this Plan
BibleProject ilibuni Tafakari ya Ujio wa Yesu ili kuhamasisha watu mmoja mmoja, vikundi vidogo vidogo, na familia kusherehekea majilio, au kuwasili kwa Yesu. Mwongozo huu wa wiki nne unashirikisha video za kikatuni, mihutasari mifupi, na maswali ya kutafakari ili kuwasaidia washiriki kuchunguza maana ya Biblia ya tumaini, amani, furaha, na upendo. Chagua mwongozo huu ili kujifunza jinsi maadili haya manne yamefika ulimwenguni kupitia kwa Yesu.
More