YouVersion Logo
Search Icon

Soma Biblia Kila Siku Julai 2021Sample

Soma Biblia Kila Siku Julai 2021

DAY 11 OF 31

Je, unajua kuwa Mungu ndiye aliyetuweka duniani kwa makusudi yake? Tunapokuwa tunayaacha mapenzi yake na kufanya vinginevyo, haachi kutuonya kwa Neno lake. Nabii Ezekieli anakumbushwa tena kuwa yeye ni kama mlinzi wa ukuta wa jiji. Wajibu wake ni kuwaonya watu wakati wowote aonapo hatari ikitokea. Haijalishi kama watu watajali kazi yake au hawatajali, Ezekieli kama mlinzi anawajibika kutimiza wajibu wake. Je, wewe unao wajibu gani? Timiza wajibu wako kama alivyokukusudia Mungu.

Day 10Day 12