YouVersion Logo
Search Icon

Soma Biblia Kila Siku Julai 2021Sample

Soma Biblia Kila Siku Julai 2021

DAY 14 OF 31

Kazi ya uchungaji siyo mali ya hao wachungaji wenyewe. Ni mali ya Mungu, na inabidi itendeke kwa mapenzi yake. Viongozi wa Israeli walitakiwa kutunza watu wa kundi lao. Badala yake, waliwanyonya ili kujinufaisha kwa faida yao. Hata waliruhusu watu kushambuliwa na kutawanywa na maadui. Kwa kuwa Mungu ni mchungaji mwema, anasema, Mimi mwenyewe nitawatafuta kondoo wangu na kuwatunza (m.11 BHN). Atawakomboa na kuwarudisha kwake. Basi, tukubali kuongozwa na huyo Mchungaji Mwema, ambaye ni sawa na Yesu. Kumbuka anavyojitambulisha katika Yn 10:11, Mimi ndimi mchungaji mwema. Mchungaji mwema huutoa uhai wake kwa ajili ya kondoo.

Day 13Day 15