YouVersion Logo
Search Icon

Soma Biblia Kila Siku Julai 2021Sample

Soma Biblia Kila Siku Julai 2021

DAY 17 OF 31

Mungu ndiye Mungu wa faraja yote (2 Kor 1:3). Ndivyo tuonavyo katika somo la leo. Waisraeli wako uhamishoni huko Babeli, na baadhi ya mataifa jirani wamejigawia nchi walimokaa. Lakini nchi hiyo ni mali yake Mungu, wala hatavumilia dharau za maadui hao. Kupitia unabii juu ya milima ya Israeli, Nabii anawahakikishia Waisraeli wamtegemee Mungu. Atageuza kabisa hali hiyo mbaya, na itakuwa njema. Msiogope, enyi kundi dogo; kwa kuwa Baba yenu ameona vema kuwapa ule ufalme (Lk 12:32).

Day 16Day 18