YouVersion Logo
Search Icon

Soma Biblia Kila Siku Mei 2021Sample

Soma Biblia Kila Siku Mei 2021

DAY 8 OF 31

Yesu akawauliza, Ni halali siku ya sabato kutenda mema, au kutenda mabaya? kuponya roho au kuiua? Wakanyamaza (m.4). Sabato kwa Wayahudi ni kama Jumapili ilivyo kwetu, yaani, siku ya kumwabudu Mungu na siku ya kupumzika. Kama Mwana wa Mungu, Yesu alijua maana ya sabato kuliko mtu mwingine. Ndiye Bwana wa sabato (2:28). Na kuhusu uhusiano wa sabato na mwanadamu, mafundisho yake ni wazi: Sabato ilifanyika kwa ajili ya mwanadamu, si mwanadamu kwa ajili ya sabato (2:27)! Lakini Mafarisayo walifungwa na mapokeo ya wazee hata wasiweze kulifurahia tendo jema (ling. m.5-6 tunaposoma: Yesu akawakazia macho pande zote kwa hasira, akiona huzuni kwa ajili ya ugumu wa mioyo yao [hapo waliponyamaza Yesu alipowauliza kama ni halali kutenda mema siku ya sabato], akamwambia yule mtu, Nyosha mkono wako. Naye akaunyosha; mkono wake ukawa mzima tena. Mara wakatoka wale Mafarisayo, wakawa wakifanya shauri juu yake pamoja na Maherodi, jinsi ya kumwangamiza.

Scripture

Day 7Day 9