YouVersion Logo
Search Icon

Soma Biblia Kila Siku Mei 2021Sample

Soma Biblia Kila Siku Mei 2021

DAY 31 OF 31

Neno hili laweza kutufundisha mambo mawili. Kwanza ni utii kwa neno litokalo kinywani mwa Mungu. Ijapokuwa marafiki waliomtaabisha Ayubu walimhuzunisha, Mungu alipomtaka Ayubu awaombee, Ayubu alitii. Utii kwa neno la Mungu ni sharti la Biblia. Jambo la pili ni kuwaombea waliotukosea. Hili nalo ni takwa la kimungu na kutusaidia kushinda mafarakano. Yesu asema: Nawaambia ninyi mnaosikia, Wapendeni adui zenu, watendeeni mema wale ambao wawachukia ninyi, wabarikieni wale ambao wawalaani ninyi, waombeeni wale ambao wawaonea ninyi (Lk 6:27-28). Mambo haya mawili yalikuwa msingi wa Ayubu kurejeshewa ufanisi, uliokuwa umepotea. Kumbuka mambo haya na kuyaishi siku zote.

Scripture

Day 30