YouVersion Logo
Search Icon

Soma Biblia Kila Siku Mei 2021Sample

Soma Biblia Kila Siku Mei 2021

DAY 1 OF 31

Mwanzo wa Injili ya Yesu Kristo, Mwana wa Mungu (m.1). ”Injili” maana yake ni "habari njema". Kuja kwa Yesu Kristo kulikuwa mpango wa Mungu tangu awali. Kwa hiyo manabii wa A/K walitabiri juu ya jambo hili. Kwa mfano katika m.2-3 Marko ananukuu “kama ilivyoandikwa katika nabii Isaya” (Isa 40:3) na Malaki (Mal 3:1). Fikiria jinsi inavyokuwa Rais anapotangaza kuzuru mahali fulani. Maandalio ya kumpokea ni mengi, barabara zinatengenezwa n.k. Kabla Yesu Kristo mwenyewe hajaja alitangulia mtu wa kumtengenezea njia. Yohana Mbatizaji alikuwa chombo teule cha Mungu cha kuwaandaa watu kiroho. Yohana alitokea, akibatiza nyikani, na kuuhubiri ubatizo wa toba liletalo ondoleo la dhambi. Wakamwendea nchi yote ya Uyahudi, nao wa Yerusalemu wote, wakabatizwa katika mto wa Yordani, wakiziungama dhambi zao (m.4-5).

Scripture

Day 2