Soma Biblia Kila Siku Mei 2021Sample
Hakuna mtu ashonaye kiraka cha nguo mpya katika vazi kuukuu (m.21). Maana yake ni kwamba Yesu amekuja na mambo mapya. Mafarisayo (m.18) ni kundi la kidini la Kiyahudi. Walijiona kuwa wafuasi halisi wa dini ya Kiyahudi. Walikuwa na mkazo wa kuifuata sheria ya Musa kwa jinsi ilivyofafanuliwa katika mapokeo ya wazee. Hayo mapokeo Yesu aliyakataa, kwa mfano sheria zile walizozitunga wenyewe kuhusu kufunga na kushika sabato. Alipoulizwa, Kwani wanafunzi wa Yohana na wanafunzi wa Mafarisayo hufunga, bali wanafunzi wako hawafungi? Yesu akawaambia, Walioalikwa arusini wawezaje kufunga maadamu bwana-arusi yupo pamoja nao? Muda wote walipo na bwana-arusi pamoja nao hawawezi kufunga. Lakini siku zitakuja watakapoondolewa bwana-arusi, ndipo watakapofunga siku ile (m.18-20). Na Mafarisayo walipomwambia Yesu, Tazama, mbona wanafanya lisilokuwa halali siku ya sabato? Akawaambia, Hamkusoma popote alivyofanya Daudi, alipokuwa ana haja, na kuona njaa, yeye na wenziwe? Jinsi alivyoingia katika nyumba ya Mungu, zamani za kuhani mkuu Abiathari, akaila mikate ile ya Wonyesho, ambayo si halali kuliwa ila na makuhani, akawapa na wenziwe? Akawaambia, Sabato ilifanyika kwa ajili ya mwanadamu, si mwanadamu kwa ajili ya sabato. Basi Mwana wa Adamu ndiye Bwana wa sabato (m.23-28). Kwake haya yalikuwa ni kama vazi kuukuu. Ila sheria ya Musa aliithibitisha, akisema: Msidhani ya kuwa nalikuja kuitangua torati au manabii; la, sikuja kutangua, bali kutimiliza. Kwa maana, amin, nawaambia ,Mpaka mbingu na nchi zitakapoondoka,yodi moja wala nukta moja ya torati haitaoondoka ,hata yote yatimie. Basi mtu ye yote atakayevunja amri moja katika hizi zilizo ndogo, na kuwafundisha watu hivyo, ataitwa mdogo kabisa katika ufalme wa mbinguni; bali mtu atakayezitenda na kuzifundisha, huyo ataitwa mkubwa katika ufalme wa mbinguni. Maana nawaambia ya kwamba, Haki yenu isipozidi hiyo haki ya waandishi na Mafarisayo, hamtaingia kamwe katika ufalme wa mbinguni (Mt 5:17-20).
Scripture
About this Plan
Soma Biblia Kila Siku Mei 2021 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha Marko na Ayubu. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Karibu kujiunga na mpango huu
More