YouVersion Logo
Search Icon

Soma Biblia Kila Siku Mei 2021Sample

Soma Biblia Kila Siku Mei 2021

DAY 12 OF 31

Taa ni mfano wa Yesu juu ya ufalme wa Mungu. Tunaweza kugawa somo kwa namna ifuatayo: Kwanza Yesu anazidi kusisitiza namna ya kulisikia neno hilo (m.21-25). Halafu anaonyesha nguvu ya hilo neno (m.26-29). Kisha anafananisha ufalme wa Mungu na mbegu ya haradali (m.30-32). Haradali ni kiungo katika vyakula. Ni mbegu ndogo sana, lakini mti wake ni mkubwa sana. Agizo la Yesu la kueneza Injili walipewa watu wachache sana (ling. Mk 16:14-15 inavyoeleza kwamba baadaye [Yesu] akaonekana kwa wale kumi na mmoja walipokuwa wakila, akawakemea kwa kutokuamini kwao na ugumu wa mioyo yao, kwa kuwa hawakuwasadiki wale waliomwona alipofufuka katika wafu. Akawaambia, Enendeni ulimwenguni mwote, mkaihubiri Injili kwa kila kiumbe). Lakini leo kuna mamilioni ya Wakristo ulimwenguni! Mfano huu unatutia moyo katika utumishi wetu.  Zingatia Gal 6:9-10: Tusichoke katika kutenda mema; maana tutavuna kwa wakati wake, tusipozimia roho. Kwa hiyo kadiri tupatavyo nafasi na tuwatendee watu wote mema; na hasa jamaa ya waaminio.

Scripture

Day 11Day 13