YouVersion Logo
Search Icon

Soma Biblia Kila Siku Mei 2021Sample

Soma Biblia Kila Siku Mei 2021

DAY 16 OF 31

Hapa twajifunza kwamba ombi la mtu si kitu kidogo kwa Yesu. Yesu aliguswa na taabu ya mtu yule, akaamua kwenda kumsaidia. Ndugu msomaji, tusikawie kumkabidhi Yesu taabu zetu tukimwomba na kumsihi atusaidie! Ila wakati mwingine inaonekana kana kwamba Yesu amechelewa kutujibu. Ndipo tunajiuliza: Je, hajatusikia au ametusahau? Ndivyo ilivyokuwa siku hiyo. Yule binti akafa kabla Yesu hajaja, kama ilivyoelezwa katika m.35, Wakaja watu kutoka kwa yule mkuu wa sinagogi, wakisema, Binti yako amekwisha kufa; kwani kuzidi kumsumbua mwalimu? Ila angalia jibu la Yesu: Usiogope, amini tu! (m.36). Hii itutie moyo kumtwika fadhaa zetu zote.



Scripture

Day 15Day 17