BibleProject | Safari ya Kujifunza Kutoka Luka Na MatendoSample

Baada ya kubatizwa kwa Yesu, anakwenda nyikani kwa siku arobaini bila chakula. Yesu anarudia safari ya wana wa Israeli ya miaka arobaini nyikani, ambako walinung'unika na kumwasi Yehova. Lakini ambapo Israeli ilifeli, Yesu anafaulu. Anapojaribiwa, Yesu anakataa kutumia uungu wake kwa manufaa yake binafsi ila badala yake anaamua kupitia changamoto na mateso wanayopitia wanadamu. Anamwamini Yehova kwa yote na anathibitisha kuwa yeye ndiye atakayeondoa maumivu na kuteseka kwa kwa Isaraeli na wanadamu wote.
Baada ya haya, Yesu anarejea kwenye mji wa kwao wa Nazareti. Anakwenda kwenye sinagogi anakoombwa asome Maandiko ya Kiebrania. Anafungua hati ya kale iliyoandikwa na Isaya, anaisoma na kuketi kisha anaongeza kwa kusema, “Leo maandiko haya yametimia mkisikia.” Waliokuwepo wanashangazwa na wanamkazia macho. Yeye ndiye aliyetabiriwa na Isaya––mtiwa-mafuta anayeleta habari njema kwa maskini, anayewaponya wagonjwa na kuwaheshimisha waliodharauliwa. Yeye ndiye atakayeleta Ufalme wake kwa njia ya kipekee, ili kurekebisha yasiyofaa na kuufanya ulimwengu kuwa wenye haki tena.
About this Plan

Safari ya Kujifunza Kutoka Luka Na Matendo huwahimiza watu, vikundi vidogo, na familia kusoma vitabu vya Luka na Matendo ya Mitume kwa siku 40. Mpango huu unajumuisha video zilizohuishwa na mihtasari ili kuwasaidia washiriki kukutana na Yesu. Na kujifunza kutoka kwenye usanifu mwema wa kifasihi wa Luka na mtiririko wa mawazo.
More
Related Plans

God Is Not ChatGPT

Sustenance (S3-E8)

Here and Now: Embracing the Gift of Presence in Marriage

Make It Happen!

Secure & Sent: Leadership for Church Planters

Seek God Passionately

Heart Detox: The War for Your Soul by Vance K. Jackson

Gone Fishin' Eight

What Makes a Good Person?
