YouVersion Logo
Search Icon

BibleProject | Safari ya Kujifunza Kutoka Luka Na MatendoSample

BibleProject | Safari ya Kujifunza Kutoka Luka Na Matendo

DAY 7 OF 40

Baada ya kusoma mafundisho ya Yesu kuhusu Ufalme wake wa kipekee, huenda tukaanza kuhoji ukuu wa “mfalme aliyefundisha kuwa mtu akupigaye shavu la kuume, mgeuzie na la pili”. Lakini tambua kuwa neema ya Yesu si udhaifu. Tunapoendelea kusoma, tunaona kwamba Mfalme Yesu ana uwezo wa kuwafufua hata wafu.

Watu wengi wanaomwona na kumsikia Yesu akitenda miujiza hii yote ya kushangaza wanafahamu kuwa ni kupitia nguvu ya Mungu. Lakini Yohana Mbatizaji hawezi kuona wala kusikia yote yanayoendelea akiwa gerezani. Yohana anaanza kuwa na wasiwasi ikiwa kweli Yesu ndiye Masihi. Yesu anatuma ujumbe kwa Yohana kwa kumnukuu tena nabii Isaya: “maskini wanahubiriwa habari njema.” Yohana anajua kuwa neno hili linamrejelea Masihi anayetarajiwa. Lakini pia anafahamu kuwa vifungu vinavyofuata kwenye maandiko ya Isaya vinatabiri kuwa Masihi atanena “uhuru kwa waliofungwa,” iweje Yohana bado ni mfungwa? Je, Yesu alimsahau? Yesu anaona dhiki ya Yohana na anatoa ahadi, “amebarikiwa asiyechukizwa nami.”

Lakini wengi wanakosa kuipokea baraka hii na wanaghadhabishwa na Yesu, hasa viongozi wa dini. Hawaelewi kwa nini Yesu ni mkarimu kwa watu wa nje ambao maisha yao ni ya kuchukiza. Lakini Yesu anajua jinsi ya kuwarekebisha wanapoletwa kwake. Kwa mfano, Luka anasimulia kuwa mwanamke yule kwenye karamu anaponyenyekea na kuipangusa miguu ya Yesu huku akimdondoshea machozi ya shukrani, Yesu anatakasa maisha yake yote kupitia msamaha wake. Na yuko tayari pia kutusamehe tunapomwendea.

Huu ndio Ufalme wa kipekee––tofauti kabisa na mambo yalivyo kawaida. Huenda tunatarajia kuwa makosa yetu yatatutenganisha na mfalme, ila Yesu sio kama wafalme wengine. Ni mwenye neema na fadhili––hata kifo na kuta za gereza haziwezi kuwatenganisha watu wake na upendo wake.

Day 6Day 8

About this Plan

BibleProject | Safari ya Kujifunza Kutoka Luka Na Matendo

Safari ya Kujifunza Kutoka Luka Na Matendo huwahimiza watu, vikundi vidogo, na familia kusoma vitabu vya Luka na Matendo ya Mitume kwa siku 40. Mpango huu unajumuisha video zilizohuishwa na mihtasari ili kuwasaidia washiriki kukutana na Yesu. Na kujifunza kutoka kwenye usanifu mwema wa kifasihi wa Luka na mtiririko wa mawazo.

More