YouVersion Logo
Search Icon

BibleProject | Safari ya Kujifunza Kutoka Luka Na MatendoSample

BibleProject | Safari ya Kujifunza Kutoka Luka Na Matendo

DAY 8 OF 40

Luka anatueleza kwamba Yesu anaanza kutangaza Ufalme wa Mungu mijini na vijini. Lakini badala ya kusafiri kwa msafara wa kifalme kama mfalme wa kawaida, Yesu anasafiri na wanafunzi wake kumi na wawili wasio na hadhi ya juu pamoja na wanawake aliowaponya na kuwaweka huru. Na wanaombatana na Yesu sio wafuasi tu; pia ni watendakazi pamoja naye. Wale walioipokea habari njema ya Yesu, ukombozi na uponyaji ndio walioieneza injili kutoka mji mmoja hadi mwingine.

Walikabiliwa na matatizo mengi walipokuwa safarini. Yesu anatuliza dhoruba, anamkomboa mtu kutokana na maelfu ya mapepo, anamponya mwanamke aliyekuwa amepinda mgongo kwa miaka kumi na miwili, anamfufua msichana wa miaka kumi na miwili na anawalisha maelfu ya watu kwa kutumia chakula alichobeba mvulana mmoja––baada ya watu wote kula, chakula kilichobaki kilijaa kwenye vikapu kumi na viwili!

Unaposoma kifungu cha leo, gundua jinsi Luka anavyorudia neno “kumi na mbili” mara kadhaa. Kumbuka, Yesu aliwachagua kimakusudi wanafunzi kumi na wawili kuonyesha kuwa anafanya mageuzi ya makabila kumi na mawili ya Israeli. Luka anaangazia hili, hivyo anarudia neno “kumi na mbili” mara kumi na mbili kwenye simulizi yake ya Injili. Kila anapotumia neno hili, anaonyesha njia nyingine ambayo Yesu anakomboa makabila kumi na mawili ya Israeli, na kupitia Israeli, anakomboa ulimwengu wote.

Mungu aliahidi kwamba kupitia makabila kumi na mawili ya Israeli mataifa yote yatabarikiwa, na Mungu aliwaita Israeli kuwa nuru kwa mataifa yote. Israeli hawakutimiza amri waliyopewa, lakini Mungu ni mwaminifu kutimiza ahadi zake. Yesu anakuja kurejesha mwito wa Israeli wa kuwa baraka kwa ulimwengu, na anafanya hivyo kwa kuwatuma wanafunzi wake kumi na wawili kutangaza Ufalme wa Mungu.

Day 7Day 9

About this Plan

BibleProject | Safari ya Kujifunza Kutoka Luka Na Matendo

Safari ya Kujifunza Kutoka Luka Na Matendo huwahimiza watu, vikundi vidogo, na familia kusoma vitabu vya Luka na Matendo ya Mitume kwa siku 40. Mpango huu unajumuisha video zilizohuishwa na mihtasari ili kuwasaidia washiriki kukutana na Yesu. Na kujifunza kutoka kwenye usanifu mwema wa kifasihi wa Luka na mtiririko wa mawazo.

More