YouVersion Logo
Search Icon

BibleProject | Safari ya Kujifunza Kutoka Luka Na MatendoSample

BibleProject | Safari ya Kujifunza Kutoka Luka Na Matendo

DAY 13 OF 40

Kwenye sehemu hii inayofuata ya kitabu cha Luka, Yesu anasimulia simulizi inayoonyesha jinsi Ufalme wake unavyogeuza mambo ulimwenguni kwa njia ya kipekee, hii hapa simulizi yenyewe.

Kuna tajiri mmoja mwenye mavazi ya bei ghali na ana nyumba yenye lango. Na kuna maskini mmoja mwenye vidonda, aitwaye Lazaro, anayeketi kwenye lango la yule tajiri, naye anatamani siku zote kula makombo yaliyoanguka kwenye meza ya yule tajiri. Lakini yule tajiri hampi chochote, na hatimaye wote wanakufa. Lazaro anapelekwa mahali pa faraja ya milele, naye yule tajiri anapelekwa mahali pa mateso. Kwa namna fulani tajiri yule anaweza kumwona Lazaro, anapomwona, anaomba Lazaro atumwe ampe maji ili yamtulize. Lakini tajiri anaambiwa kuwa haiwezekani, kisha anakumbushwa kuhusu maisha yake ulimwenguni, jinsi alivyoishi maisha ya raha naye Lazaro alihitaji msaada wake. Hivyo tajiri anaomba Lazaro atumwe kwa ndugu zake ulimwenguni awaonye ili wasije wao pia wakafika mahali pa mateso. Lakini anaelezwa kuwa jamaa zake wameonywa vya kutosha kupitia maandiko ya manabii wa Kiebrania. Tajiri yule anasisitiza kuwa Lazaro akifufuka kutoka kwa wafu jamaa zake watashawishika. Lakini anaelezwa kuwa haiwezekani. Wanaokataa kumsikiliza Musa na manabii hawatashawishika hata mtu akifufuliwa kutoka kwa wafu.

Baada ya kusimulia simulizi hii, Yesu anawaonya watu wote kuwa mateso yatawafika wale wanaofanya wengine kuteseka. Ili kuepuka mateso haya, anawafundisha watu wote kuwaajali wengine na kuwarekebisha wanaopotoka. Wanaosikiza wanaporekebishwa watasamehewa, hata ikiwa wanahitaji msamaha huo tena na tena. Yesu ni mwenye huruma. Angependa watu wote wamsikilize kabla ya muda kuyoyoma. Yesu alikuja kuondoa mateso lakini kivipi? Anafundisha ukweli na anatoa msamaha wake kidhabihu kwa wote wanaoupokea. Vilevile, wafuasi wake wanapaswa kuwafundisha wengine na kuwasamehe.

Wanafunzi wa Yesu wanayasikia haya yote na wanagundua kuwa hawamwamini Mungu kiwango cha kuwawezesha kutekeleza mafundisho ya Yesu, hivyo wanaomba kuwa na imani zaidi.

Day 12Day 14

About this Plan

BibleProject | Safari ya Kujifunza Kutoka Luka Na Matendo

Safari ya Kujifunza Kutoka Luka Na Matendo huwahimiza watu, vikundi vidogo, na familia kusoma vitabu vya Luka na Matendo ya Mitume kwa siku 40. Mpango huu unajumuisha video zilizohuishwa na mihtasari ili kuwasaidia washiriki kukutana na Yesu. Na kujifunza kutoka kwenye usanifu mwema wa kifasihi wa Luka na mtiririko wa mawazo.

More