YouVersion Logo
Search Icon

BibleProject | Safari ya Kujifunza Kutoka Luka Na MatendoSample

BibleProject | Safari ya Kujifunza Kutoka Luka Na Matendo

DAY 18 OF 40

Viongozi wa hekalu hawawezi kumuua Yesu bila ruhusa ya gavana wa Kirumi, Pontio Pilato. Kwa hivyo wanamshtaki Yesu kuwa yeye ni mfalme muasi anayechochea mapinduzi dhidi ya mtawala wa Kirumi. Pilato anamuuliza Yesu, “wewe ndiye Mfalme wa Wayahudi?” Yesu anamjibu, “Wewe wasema.” Pilato anaweza kuona kuwa Yesu hana hatia na hastahili kifo, lakini viongozi wa kidini wanasisitiza kwamba yeye ni hatari. Kwa hivyo baada ya Yesu kupelekwa kwa Herode kisha kurudishwa kwa Pilato akiwa amejeruhiwa na anatokwa na damu, Pilato na viongozi wa kidini wanakubaliana jambo la kushangaza. Pilato atamwachilia muasi halisi wa Rumi, anayeitwa Baraba, badala ya Yesu. Asiye na makosa anahukumiwa badala ya mwenye hatia.

Yesu anachukuliwa pamoja na wahalifu wengine wawili walioshtakiwa na anasulubiwa kwa misumari kwenye msalaba wa Warumi. Kifo chake kinafanywa hadharani. Watu wanapiga mnada nguo zake na kumdhihaki wakisema, “ikiwa wewe ndiye Mfalme wa masihi, jiokoe!” Lakini Yesu anawapenda adui zake hadi mwisho. Anawaombea msamaha waliomsulubisha na anampa tumaini mmoja wa wahalifu waliosulubishwa pamoja naye akisema, “Leo utakuwa nami paradiso.”

Ghafla giza linafunika nchi yote, pazia la hekalu linapasuka katikati, na Yesu anamlilia Mungu kwa pumzi yake ya mwisho, “mikononi mwako naiweka roho yangu.” Jemadari wa Kirumi anashuhudia haya yote na kusema, “hakika mtu huyu alikuwa mwenye haki.”

Scripture

Day 17Day 19

About this Plan

BibleProject | Safari ya Kujifunza Kutoka Luka Na Matendo

Safari ya Kujifunza Kutoka Luka Na Matendo huwahimiza watu, vikundi vidogo, na familia kusoma vitabu vya Luka na Matendo ya Mitume kwa siku 40. Mpango huu unajumuisha video zilizohuishwa na mihtasari ili kuwasaidia washiriki kukutana na Yesu. Na kujifunza kutoka kwenye usanifu mwema wa kifasihi wa Luka na mtiririko wa mawazo.

More