BibleProject | Safari ya Kujifunza Kutoka Luka Na MatendoSample
Kabla hatujaanza somo la leo, hebu tuchambue sura ya tisa, ambapo Luka anafunua mpango wa kushangaza wa Yesu kutawala Israeli kwa kuwa mtumishi mwenye kuteseka anayerejelewa katika kitabu cha Isaya sura ya 53. Luka anatuambia jinsi Eliya na Musa walizungumza na Yesu kuhusu kuondoka kwake au “kutoka.” Yesu ndiye Musa wa kizazi hiki, ambaye kupitia kutoka kwake (kifo), ataikomboa Israeli kutoka kwenye utawala wa dhambi na uovu wote. Baada ya ufunuo huu wa kushangaza, Luka anaanza simulizi kuhusu safari ndefu ya Yesu kwenda mji mkuu kwa ajili ya Pasaka, ambako atakufa ili atawazwe kuwa Mfalme wa kweli wa Israeli.
Basi sasa, tukiangazia sura ya 22 leo, tunaona kuwa Yesu amewasili Yerusalemu kusherehekea sikukuu ya Pasaka ya kila mwaka──maadhimisho ya Kiyahudi ya kusherehekea jinsi Mungu alivyowakomboa wana wa Israeli kutoka utumwani. Yesu anapowakusanya wanafunzi wake kumi na wawili kwa chakula cha kawaida cha Pasaka, anafafanua maana ya mkate na kikombe kwa njia ambayo wanafunzi wake hawakuwahi kusikia, lakini maana yenyewe ndiyo inayoashiriwa kwenye simulizi ya Kutoka. Anawaeleza wanafunzi wake kuwa mkate uliovunjwa unaashiria mwili wake nayo divai inaashiria damu yake, ambayo itaanzisha agano jipya kati ya Mungu na Israeli. Katika hili, Yesu anatumia sakramenti ya Pasaka kueleza maana ya kifo chake kinachokuja, lakini wanafunzi wake hawaelewi. Hapo wanaanza kubishana kwenye meza kuhusu ni nani atakayekuwa mkuu zaidi katika Ufalme wa Mungu, na baadaye usiku huo wanalala badala ya kuomba pamoja na Yesu. Mmoja wa wanafunzi hao kumi na wawili anashiriki katika mauaji ya Yesu, na mwanafunzi mwingine anamkana Yesu.
Scripture
About this Plan
Safari ya Kujifunza Kutoka Luka Na Matendo huwahimiza watu, vikundi vidogo, na familia kusoma vitabu vya Luka na Matendo ya Mitume kwa siku 40. Mpango huu unajumuisha video zilizohuishwa na mihtasari ili kuwasaidia washiriki kukutana na Yesu. Na kujifunza kutoka kwenye usanifu mwema wa kifasihi wa Luka na mtiririko wa mawazo.
More