YouVersion Logo
Search Icon

BibleProject | Safari ya Kujifunza Kutoka Luka Na MatendoSample

BibleProject | Safari ya Kujifunza Kutoka Luka Na Matendo

DAY 19 OF 40

Luka anatueleza kuhusu baadhi ya wanawake waliomfuata Yesu alipokuwa hai. Wanauona mwili wa Yesu ukiwa umewekwa kaburini siku ya kuuawa kwake, na wanarudi asubuhi ya siku inayofuata Sabato, mapema iwezekanavyo. Lakini wanapofika, wanakuta kaburi likiwa wazi na tupu. Hawafahamu mwili wa Yesu umekwenda wapi, na ghafla malaika wawili waliovaa nguo za kumeta-meta wanawatokea na kuwaambia kuwa Yesu yu hai. Wanashangaa. Wanakimbia na kuwaambia wanafunzi wengine kila kitu ambacho wameona, lakini ripoti yao inachukuliwa kuwa upumbavu na hamna anayewaamini.

Wakati huo huo, nje ya Yerusalemu watu wawili miongoni mwa wafuasi wa Yesu walikuwa wanaondoka mjini kuelekea mji wa Emau. Wanazungumza kuhusu yaliyotukia wiki ya Pasaka kisha Yesu anakaribia na kuongozana nao lakini hawamfahamu. Yesu anazungumza nao na kuwauliza wanachozungumzia. Wanasimama, wanafedheheshwa na mazungumzo hayo na kushangaa kwamba hakuwa anafahamu yaliyotokea siku chache zilizopita. Wanamwambia wanamzungumzia Yesu, nabii mwenye uwezo waliyedhani kuwa angeiokoa Israeli lakini akauawa. Wanamwambia jinsi kuna wanawake wanaoshuhudia kuwa yuko hai, lakini wao hawajui cha kuamini. Kwa hivyo Yesu anawaeleza kuwa hilo ndilo limekuwa likiashiriwa kwenye Maandiko ya Kiyahudi. Israeli ilihitaji Mfalme atakayeteseka na kufa kama muasi kwa niaba ya waasi wote. Mfalme huyu angethibitika kupitia ufufuo wake ili kutoa uzima wa kweli kwa wale wanaoupokea. Lakini wasafiri hawa bado hawaelewi. Wamekanganyika sana na wanamsihi Yesu akae nao kwa muda zaidi. Hili linatupeleka kwenye tukio ambapo Luka anatueleza jinsi Yesu alivyoshiriki nao chakula. Anautwaa mkate, anaubariki, anaumega na kuwapa kama alivyofanya kwenye karamu ya mwisho kabla ya kifo chake. Hii inaashiria jinsi mwili wake ulivyovunjwa, yaani kifo chake msalabani. Na wanapokula mkate uliomegwa macho yao yanafunguliwa ili wamwone Yesu. Hiki ni kisa kuhusu ugumu wa kumtambua Yesu ni nani. Je, iweje nguvu za kifalme na upendo wa Mungu vidhihirishwe kupitia kifo cha aibu cha mtu huyu? Je, mtu mnyenyekevu anawezaje kuwa Mfalme wa ulimwengu kupitia udhaifu na kujitoa kama dhabihu? Ni vigumu sana kuelewa! Lakini huu ndio ujumbe wa Injili ya Luka. Mawazo yetu yanahitaji kufanywa upya ili tuweze kuelewa na kuupokea Ufalme wa kipekee wa Yesu.

Scripture

Day 18Day 20

About this Plan

BibleProject | Safari ya Kujifunza Kutoka Luka Na Matendo

Safari ya Kujifunza Kutoka Luka Na Matendo huwahimiza watu, vikundi vidogo, na familia kusoma vitabu vya Luka na Matendo ya Mitume kwa siku 40. Mpango huu unajumuisha video zilizohuishwa na mihtasari ili kuwasaidia washiriki kukutana na Yesu. Na kujifunza kutoka kwenye usanifu mwema wa kifasihi wa Luka na mtiririko wa mawazo.

More