BibleProject | Safari ya Kujifunza Kutoka Luka Na MatendoSample
Tunapoelekea kwenye sura zinazofuata za kitabu cha Luka, hebu tukumbuke maneno ya Yesu baada ya kusoma maandiko ya Isaya. Yesu ndiye aliyekuwa akirejelewa na Isaya tangu mwanzo. Yeye ndiye mtiwa mafuta atakayeleta habari njema kwa maskini, atakayewaponya waliovunjika moyo na kuwakomboa mateka.
“Leo maandiko haya yametimia,” Yesu alisema. Simulizi inayofuata tamko hili inaonyesha matendo yanayohusiana na habari njema za Yesu. Katika sehemu hii ya kitabu cha Luka, tunaiona habari njema ya Yesu pale anapowawezesha wavuvi waliochoka kupata samaki, kumponya mtu mwenye ukoma, kumsamehe mtu aliyepooza na kumhusisha mtoza ushuru aliyedharauliwa na jamii katika huduma yake. Yote haya yanasababisha uhasama kati yake na vikundi vya kidini, na zaidi ya hayo, Yesu anamponya mtu mwenye mkono uliopooza siku ya Sabato, siku ya kupumzika. Sasa viongozi wa dini wameghadhabishwa. Hawaelewi kwa nini Yesu anavunja sheria zao za Kiyahudi za Sabato na anajihusisha na watu wasioheshimika.
Lakini Yesu anawatetea wanyonge na anawafafanulia viongozi wa kidini kiini cha sheria ya Kiyahudi na anawaeleza kuhusu Ufalme wake ulivyo wa kipekee. Anawaeleza kuwa yeye ni kama tabibu anayewashughulikia walio wagonjwa sio wenye afya. Anaweka wazi kuwa siku ya sabato inahusu urejesho kwa wanaoumia. Yesu ndiye anayerejesha. Hawachagui walio wakuu kwenye jamii; badala yake, anarejesha hadhi ya wanaoteseka. Na wanaoteseka wanapomfuata, wanapata urejesho na wanajiunga naye kwenye kazi yake.
Scripture
About this Plan
Safari ya Kujifunza Kutoka Luka Na Matendo huwahimiza watu, vikundi vidogo, na familia kusoma vitabu vya Luka na Matendo ya Mitume kwa siku 40. Mpango huu unajumuisha video zilizohuishwa na mihtasari ili kuwasaidia washiriki kukutana na Yesu. Na kujifunza kutoka kwenye usanifu mwema wa kifasihi wa Luka na mtiririko wa mawazo.
More