YouVersion Logo
Search Icon

Soma Biblia Kila Siku 10/2020Sample

Soma Biblia Kila Siku 10/2020

DAY 9 OF 31

Hatujui kwa hakika mwiba uliokuwamo mwilini mwa Paulo ulikuwa ni nini? Lakini kwa vyovyote vile lilikuwa ni tatizo sugu, lililomsumbua mtume huyu na huduma yake. Badala ya kuliondoa tatizo, Mungu alimpa nguvu za kukabiliana nalo. Zingatia m.8-9: Kwa ajili ya kitu hicho nalimsihi Bwana mara tatu kwamba kinitoke.Naye akaniambia, Neema yangu yakutosha; maana uweza wangu hutimilika katika udhaifu. Basi nitajisifia udhaifu wangu kwa furaha nyingi, ili uweza wa Kristo ukae juu yangu. Majaribu yajapo yasituondoe katika uwepo wa Mungu. Badala yake yatuweke karibu na Mungu wetu. Ni ushuhuda wa Paulo kwamba ndivyo yanavyofanya: Kwa hiyo napendezwa na udhaifu, na ufidhuli, na misiba, na adha, na shida, kwa ajili ya Kristo. Maana niwapo dhaifu ndipo nilipo na nguvu (m.10; pia unaweza kusoma Rum 8:31-39). Kumtegemea Mungu katika kila hali hujenga na kuimarisha tabia ya Kikristo na ya utii. Yesu ni mfano wake hasa (soma k.m. Lk 22:39-46).

Day 8Day 10

About this Plan

Soma Biblia Kila Siku 10/2020

Soma Biblia Kila Siku 10/20 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha 2 Wakorintho, Mwanzo na 1 Petro. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Karibu kujiunga na mpango huu

More