Soma Biblia Kila Siku 10/2020Sample
Hapa mtume Paulo anatetea mamlaka yake ya kuhubiri Injili ambayo yametoka kwa Kristo. Wakristo walikuwa na mashaka na hata maswali juu ya uhalali wa utume wake. Paulo anajitetea kwa sababu ya Injili, si ili kujinufaisha yeye binafsi. Wakati unaingia na kuingizwa majaribuni, je, unafikiria juu ya heshima au hadhi yako tu au unajihusisha zaidi na jinsi watu watakavyomtambua na kumfikiria Yesu Kristo? Usijitazame wewe, mtazame Yesu Kristo. Tuweke kando kila mzigo mzito, na dhambi ile ituzingayo kwa upesi; na tupige mbio kwa saburi katika yale mashindano yaliyowekwa mbele yetu,tukimtazama Yesu, mwenye kuanzisha na mwenye kutimiza imani yetu(Ebr 12:1-2).
Scripture
About this Plan
Soma Biblia Kila Siku 10/20 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha 2 Wakorintho, Mwanzo na 1 Petro. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Karibu kujiunga na mpango huu
More