Soma Biblia Kila Siku 10/2020Sample
Jijaribuni wenyewe kwamba mmekuwa katika imani; jithibitisheni wenyewe: Au hamjijui wenyewe, kwamba Yesu Kristo yu ndani yenu?(m.5). Wakristo wa Korintho walikumbushwa kujipima na kijithibitisha wenyewe ili kujua hali yao ya kiroho. Watajipimaje? Ni kwa njia ya kumtazama Kristo, kulisoma na kujifunza Neno la Kristo. Kujichunguza maisha yetu ya kiroho ni jambo jema na zuri sana. Tazama k.m. wimbo katika kitabu cha Tumwabudu Mungu wetuusemao: "Uchunguze ndani yangu", au wimbo katika Tenzi za Rohoniusemao: "Peleleza ndani yangu". Kama ambavyo tunajichunguza afya zetu za mwili na akili hospitalini, tusiache kuchunguza afya zetu za kiroho.
Scripture
About this Plan
Soma Biblia Kila Siku 10/20 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha 2 Wakorintho, Mwanzo na 1 Petro. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Karibu kujiunga na mpango huu
More