Soma Biblia Kila Siku 10/2020Sample
Tunazidi kufundishwa juu ya mwenendo wetu. Anatuagiza tupendane kwa moyo(m.22)! Ila kila wakati hachoki pia kutukumbusha juu ya wokovu wa Mungu katika Kristo. Maana hujua kwamba nguvu ya kuishi maisha mapya hatunayo sisi wenyewe. Nguvu ya Roho twapata tena na tena tunapomfikiria Yesu Kristo jinsi alivyotufia msalabani, na jinsi alivyofufuka (m.2-3, 11, 18-19, 21 na 23)! Lazima tuhubiriwe Kristo na damu yake tena na tena ili tujazwe na Roho wa Kweli! Kwa sababu neno la msalaba kwao wanaopotea ni upuzi, bali kwetu sisi tunaookolewa ni nguvu ya Mungu (1 Kor 1:18). Ninyi Wagalatia msio na akili, ni nani aliyewaloga, ninyi ambao Yesu Kristo aliwekwa wazi mbele ya macho yenu ya kuwa amesulibiwa?Nataka kujifunza neno hili moja kwenu. Je! Mlipokea Roho kwa matendo ya sheria, au kwa kusikia kunakotokana na imani?Je! Mmekuwa wajinga namna hii? Baada ya kuanza katika Roho, mnataka kukamilishwa sasa katika mwili?(Gal 3:1-3)
Scripture
About this Plan
Soma Biblia Kila Siku 10/20 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha 2 Wakorintho, Mwanzo na 1 Petro. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Karibu kujiunga na mpango huu
More