Soma Biblia Kila Siku 10/2020Sample
Mungu anatupatia rasilimali nyingi ili tuzitumie na kuwekeza kwake. Mbegu ipandwapo huota, hukua na kisha huzaa. Matunda ya mbegu hii hushibisha mpandaji na wengine. Atupacho Mungu, anapenda kionekane, kisifichwe wala kupotezwa. Shabaha ya kumtolea Mungu na kusaidia wengine si ili mtoaji atajirike. Wale wapokeao sadaka au kipawa chako wanakuwa wamesaidiwa. Matokeo yake watamtukuza Mungu na watamwombea mtoaji. Kwa kubariki wengine nawe utabarikiwa. Rudia na kuzingatia m.12-15: Utumishi wa huduma hii hauwatimizii watakatifu riziki walizopungukiwa tu, bali huzidi sana kuwa na faida kwa shukrani nyingi apewazo Mungu;kwa kuwa mkijaribiwa kwa utumishi huo, wanamtukuza Mungu kwa ajili ya utii wenu katika kuikiri Injili ya Kristo, na kwa ajili ya ukarimu wenu mliowashirikisha wao na watu wote.Nao wenyewe, wakiomba dua kwa ajili yenu, wawaonea shauku kwa sababu ya neema ya Mungu iliyozidi sana ndani yenu.Mungu ashukuriwe kwa sababu ya kipawa chake, tusichoweza kukisifu kama ipasavyo.
Scripture
About this Plan
Soma Biblia Kila Siku 10/20 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha 2 Wakorintho, Mwanzo na 1 Petro. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Karibu kujiunga na mpango huu
More